Kumpa mahojiano Dudu Baya ni upuuzi.

Kumpa mahojiano Dudu Baya ni upuuzi.

Heshima ya kipaza ya chombo cha habari iko wapi?, mbona vipaza vinawekwa mbele ya watu ambao wamejaa hovyo?. Hivi kweli habari za hovyo ndiyo pendwa kwa jamii?. (Soni)

Ipi ni habari kwa Dudu Baya? Mbona haina maana wala maana yenyewe? Sasa anahojiwa nini? Na anene nini? Ili isaidie nini?. Kweli wanaweka vipaza mbele yake!!, na ili iweje? Au ni katika kuchafua biashara za watu?. (Ajabu)

Leo ambao wamekimbilia kumhoji Dudu Baya katika endelezo la kuchafua biashara za watu yapasa mjitafakari mno, kwa maana ipo siku yenu pia ataweza nena mengi zaidi upande wenu je!itakuaje? (Tafakari)

Tuligemea kuona potezeo juu ya Dudu Baya na apite mithili ya pepo za fukwe ya bahari ya hindi. Lakini kumbatio la mahojiano yake linatupa mashaka mno. (Shangazo)

Kumhoji Dudu Baya inaonyesha dhahiri yakuwa watu wa ‘Media’ hawapendani kabisa na wapo kufurahi kila jambo la mwenzao katika fedheha. (Kweli).

Kiukweli sisi haijatupendeza katika semi za Dudu Baya zenye kubomoa ukubwa majina ya watu yenye biashara kubwa kwa maana watu/mtu wametumia/ametumia nguvu, akili, na gharama katika kutengeneza jina lake iweje leo ulibomoe kwa kwa sekunde 26? (Fedheha)

Pole zetu kwa wenye uelewa mdogo ambao hawajui shabaha ya jambo hili,  na ambao watakuwa salama ni wale wenye kujipendekeza tu wenye chukizo katika kujipendekeza hakika mtafadhaishwa mno. (Chukizo)

Hakika ‘Akili ubongoni mithili ya rababendi’ na wala hatutaki kutumia semi mbaya ya mswahili juu ya Dudu Baya yakuwa “ Uzuri wa godoro wa nje tu, ndani mna pamba” (Akili).

Ni vyema wenye vipaza muhoji yenye maana, na katika maana hovyo za Dudu Baya hazina faida wa maana bali chukizo kubwa mbele ya wajuzi wenye kujua maana ya kufedheheshwa. (Naam)

Na ni vyema watu wajifunze kudharau hovyo za watu wa hovyo aina ya Dudu Baya, lakini kumbatio la hovyo la watu wa hovyo kunayo siku litaleta matata. (Tafakari)

#TuzungumzeMuziki