Kumpa Hamisa Mobetto sifa za uimbaji ni kuukosea muziki wa Bongo Fleva. (Hakika)

Kumpa Hamisa Mobetto sifa za uimbaji ni kuukosea muziki wa Bongo Fleva. (Hakika)

Hatujui ni kwanini imekuwa ni rahisi mno kwa wengi kusifiana kwa sifa za uongo tena bila hata soni mbele ya jamii ya wajuzi wa muziki. (Ajabu)

Na tumeona namna ambavyo sifa za pongezi zimekuwa nyingi katika aminisho la Hamisa ni muimbaji mzuri, ni wazi sifa hizi hazina uhalisi hata kidogo. (Chekesho)

Ingawaje kwa upana wa maana ya uimbaji inawezekana kuonanekana yakuwa Hamisa ni muimbaji kweli. Ikumbukwe kipindi hiki wengi hawajui kuhusu muziki na hawajui kama hawajui. (Maana)

‘Uimbaji’ ni kutamka maneno katika hali ya kimuziki, na huwenda kuwa juu ya ala za muziki ama katika upekee. (Acappela)

Kwa maana hiyo kila mtu ni muimbaji lakini kuimba haswa kwa upana wa ujuzi ni katika uchache mno. Na hapa ni katika kucheza na sauti zile panda shuka zenye ladha kamili.(Uhalisia) 

Hivyo kwa sasa Hamisa hana vigezo vya kuitwa muimbaji imara bali muimbaji mwenye ukawaida katika kundi la wengi. (Anajifunza)

Lakini kulingana na upana wa muziki huenda akaja kuwa muimbaji mzuri sababu muziki unahitaji mazoezi kila leo katika funzo lake. (Kabisa)

Ila sasa kusema yakuwa “Hamisa ni muimbaji imara na bora ni kuukosea muziki wa bongo fleva” (Naam) 

Kigezo cha kuwa bora ni kipi kwa Hamisa? ulaini wa sauti ama? mbona hana uwezo wa kucheza na sauti katika panda shuka zenye mvuto katika anguko la mwisho wa uimbaji ama mwanzoni. Sasa anasifiwa kipi? (Shangazo)

Uimbaji wake ni wa kiwango kidogo mno yani katika kweli yenye kweli ni uimbaji wa kawaida kuliko kawaida yenyewe. (Ndiyo)

Na tunawakumbusha yakuwa wale ambao hudhani msanii kuwa na watazamji wengi kwenye mtandao wa ‘Youtube’ ndiyo kigezo cha ubora, ni wazi hakuna kitu kama hicho katika muziki. (Kweli)

Kipimo cha ubora wa wimbo ni katika ujazo wa mashairi, mdundo, uimbaji pamoja na changanyo la ladha kamili la muziki katika usikivu. (Naam)

Je! wimbo wa My Love wa Hamisa una vigezo vya kuwa bora? au uimbaji wake wa moja kwa moja mithili ya mlevi afuatae njia ya kwenda kwake inapaswa tusifu? (Hapana)

Tuambie ukweli katika kuwekana sawa na tuweke endelezo jema la kimuziki, hatuwezi kusonga kimuziki kwa kusifu uongo wa uimbaji kama wa Hamisa. (Tuwe wa kweli)

Leo tunataka tushindane na Nigeria katika soko la kimataifa, sasa kwa kusifu uimbaji wa Hamisa tutaweza kushindana na soko la kimataifa? (Thubutu)

#MuzikiNiSisi