Kumlinganisha Young Lunya na Young Killer mnatumia vigezo gani? (Ulizo)

Kumlinganisha Young Lunya na Young Killer mnatumia vigezo gani? (Ulizo)

Imekuwa ni jambo jema sasa kwa mashabiki wengi na watu wa Media katika linganisho la Lunya na Killer. (Eeh)

Na wanafika mbali zaidi kiasi cha kunena yakuwa “Young Lunya ni bora kuliko Young Killer” (Fedheha)

Ulinganisho wao umefanya tupate swali kuu yakuwa “Wanatumia vigezo gani katika kuweka linganisho?” (Ulizo)

Maana katika kweli yenye kweli kuna mambo makuu matano katika kuweka linganisho la msanii na msanii. (Uhalisia)

Mosi ni ‘Rap Skills’ hapa tazamo ni uwezo wa msanii husika katika upana wa utunzi wa mashairi. Je! ana kiwango cha juu? na uwezo wa kubadilika upo na upana? Je! katika Rap Skills unaweza kumuweka Lunya na Killer? (Thubutu)

Pili ni ‘Consistency’ Uwezo wa kudumu kwenye muziki kwa muda mrefu tangu kufahamika kwake. Lakini ubora wa kazi na nidhamu.Je! Lunya amedumu vipi? ila nidhamu yake ya kazi mnaijua?.  (Soni)

Na tukitaja wasanii 20 bora wa HipHop Lunya anaweza kuwepo? Uhalisia ni Killer yupo katika muda mrefu tangu toka yake mpaka sasa. (Hakika)

Tatu ni ‘Body Of Work’ Katika mwili wa kazi tunatazama msanii tangu atoke ana album ngapi? Je! Ep? au Kanda Mseto?. Ilihali ana nyimbo/Video ngapi ambazo zimewahi kufanya vyema. (Eeh)

Sasa linganisho la Lunya na Killer latoka wapi? Ikiwa tu Lunya hana hata wimbo mmoja ambao umewahi kuwa katika chati yoyote ya muziki. (Fedheha)

Nne ni ‘Culture Impact’  Tazamo kuu hapa ni msanii amefanya nini ambacho kimeleta mapinduzi katika uwanja wa muziki? Je! uhalisia kati ya Lunya na Killer nani amefanya mapinduzi? (Ulizo)

Nani amegusa jamii katika mengi yenye mengi? kwa upana wa kukumbukwa katika mengi zaidi? (Tafakarini)

Tano ni ‘ Accolades’ Hii ni sifa ya tuzo haswa, ambapo ni tuzo ngapi msanii husika amewahi kupata katika sanaa yake?  (Naam)

Katika uhalisia wa vigezo vikuu vitano ni kosa na makosa kwa watu kumfananisha Young Killer na Young Lunya. Haipaswi kuwepo kwa mfanano kabisa. (Hakika)

Tuheshimu nafasi ya Young Killer katika muziki huu, lakini uchipukizi wa Lunya pia tunaufurahia, kuanza kumlinganisha na wakubwa zake ni kumvisha vazi lisilomtosha. (Uhalisia)

#MuzikiNiSisi