Kulikuwepo na ulazima wa Fid Q kujibu hovyo za Babu Tale na Fella? (Ulizo)

Kulikuwepo na ulazima wa Fid Q kujibu hovyo za Babu Tale na Fella? (Ulizo)

Mswahili hunena “Kukaa kimya ni jibu pia, tena lenye ujazo wa hekima” lakini hakuacha nena yakuwa “Mjibu mjinga kulingana na ujinga wake” (Naam)

Ila hakuacha kusisitiza yakuwa “Mjinga muweke mbele ukimuweka nyuma utamsahau” (Uhalisi). Mswahili ni mwenye hekima za uchanganyo mno. (Hakika)

Katika uhalisi na kweli yenye kweli Fid Q hana kosa katika semi zake juu ya tangazo la kubwa moja la Clouds Fm (Tigo Fiesta).

Semi ipi ni mbaya amenena pale?  Mbona ni kama watu wanamlisha semi ambazo hazifai?. Kwani Fid Q alimtaja nani na ili iweje? (Fikirio)

Na tazamo la upana katika video ya Babu Tale na Fella ni wazi limejaa fedheha katika semi mbaya juu mlengwa mhusika. (Nani)

Lakini nao hawakumtaja Fid Q katika uwazi, hivyo hakuna mwenye hakika bali ufananisho wa lugha ya picha tumizi. (Eeh)

Maana wote wawili tunanena wametupa

mawe gizani, hivyo katika uwazi hatukutaraji kwa hekima na ujuzi wa Fid Q kujibu hovyo hizo zenye tafakari ndogo zaidi ndogo yenyewe. (Kabisa)

Lakini ni vyema watu kutazama watu hawa Tale na Fella kwa umakini mkubwa mno. Leo hii Media yao ni changa mno, lakini vinywa vyao vimejaa kebehi zenye uzito.

Je! wakiwa wakubwa katika ukubwa wa Clouds Media Group itakuaje? (Hatari). 

Kama Sanaa imezaliwa upya kwanini wao viongozi wananena hovyo juu ya wasanii wengine? (Ulizo)

Je! matangazo yao katika kufungua wasanii wenye vifungo yalete matata na Clouds Media Group? (Ulizo)

Maana katika lugha ya picha ni kwamba inaamika yakuwa Clouds Media Group waliwaweka baadhi ya wasanii kifungoni. (Hapana)

Ni vyema watu watafakari katika upana, wasanii pia wajue kuwa Wasafi Festival, Mziki Mnene, Tigo Fiesta na mengineyo isifanye uharibu mahusiano yako na wengine. (Hujui kesho)

Fid Q leo yake imekuwa mbaya kwa upana, lakini kumbukukeni kumbukumbu yakuwa miezi kadhaa nyuma walikuwa katika cheko la Fresh Remix. (Leo ikoje)

Msanii fanya tamasha, usitingishwe na muandaaji yoyote wa tamasha kumbuka hiyo ni kazi yako yapasa uwepo katika yote uongeze kipato. (Shikilia)

Lakini mswahili haachi kunena yakuwa “Shika Shika lingali kichwani” Tafakariiii. 

#TuzungumzeMuziki