Kuivua hofu kuvaa ujasiri chanzo kikuu cha mafanikio ya Diamond Platnumz.

Kuivua hofu kuvaa ujasiri chanzo kikuu cha mafanikio ya Diamond Platnumz.

Mwaka 2016 tuliandika andiko lisemalo “Diamond Platnumz na maisha tofauti na wenyeji wake”

Ambapo wapo ambao walibeza maana pia tulikuwa nje ya maisha yao lakini daima kweli yenye kweli huishi.

Na sasa tunaona nguvu yake na Wasafi Festival kabla hata ya kuanza, lakini Diamond ni msanii pekee kufikiri namna ya kujikwamua kutoka kwenye utegemezi wa tamasha moja au mawili na kuwa na lake/lao.

Na amini twanena yakuwa Wasafi Festival italeta mapinduzi mema na muendelezo mwema wa muziki wetu, lakini ni kama litatazama upana wa haki na gawio la kila msanii kwa usawa wake.

Na genge ambalo yukonalo Diamond hakika ni genge lenye uchu wa mapinduzi na kuweza kushika usukani wa muziki.

Naam! watafanikiwa kwa maana wengi wanatamani kuwepo kwa matamasha mengi zaidi yenye kutoa nafasi kwa wasanii wengi si wale wale kwa upendeleo, kujuana, rushwa na kuimbishana bure tena kwa ubabe.

Na wajuzi wananena yakuwa “Muziki upo pazuri sasa sio katika uzamani wa bila fulani na fulani huendi, bali usawa katika usawa wa kila msanii kwa nafasi ya kufanya yake umefika”.

Na nguvu aliyonayo Diamond katika kueleza mengi na kufanya mengi ya juu ya sanaa hii hakika yapasa tusifu.

Mkumbuke yakuwa muziki ulikuwa mateka kwa muda mrefu, hivyo sasa walau unaanza kupata uhuru, na hakika yapasa watokee wengi katika kuleta usawa wa matamasha na mengi juu ya sanaa na si mmoja tu.

Na ngao imara ni kuivua hofu na kuvaa ujasiri hakika hakuna ambacho kinashindikana.

Naam! #TuzungumzeMuziki