Kufanikiwa kwa msanii ni uongozi au msanii mwenyewe?

Kufanikiwa kwa msanii ni uongozi au msanii mwenyewe?

Kila msanii mchanga ambaye tunakutanae amekuwa akilalama yakuwa hana uongozi (Menejimenti) ndiyo maana hawezi kufanya vyema kwenye muziki.

Sentensi hiyo imetufanya tujiulize maswali mengi lakini moja ni “Kufanikiwa kwa msanii ni uongozi au msanii mwenyewe?”

Tukitazama kwa upana sisi tutasema ni msanii mwenyewe lakini uongozi kama msanii atauongoza kwa maono yake.

Tukizungumza katika wasanii ambao wana mafanikio makubwa huwezi kuacha kumtaja msanii Diamond Platnumz.

Ambaye yeye anaonekana amezungukwa na viongozi watatu yani Babu Tale, Sallam na Mkubwa Fella.

Lakini ikumbukwe Mkubwa Fella ndiye yule yule ambaye alikuwa na genge la Tmk wanaume family lakini Yamoto Band ila tusisahau Mkubwa na wanae pamoja na Madada sita kwasasa.

Kwa upande wa Tale ni alikuwa na TipTop Connection ambayo iliundwa na Madee, Tunda Man, Cassim Mganga, Keisha, Pingu na Desso, Z anto, Pnc na wengine wengi.

Lakini katika wasanii hao wote kutoka kwa Babu Tale na Fella hawakuweza kuwafikisha walau nusu ya kiwango cha Diamond Platnumz.

Hii inatoa maana gani? Zaidi ya juhudi za msanii husika ndizo zitafanya uwepo wa kufika mbali Zaidi kimuziki.

Na hatumaanishi kama wasanii ambao walikuwa chini ya mabwana hawa hawakuwa na juhudi hapana, bali wao kulala Zaidi kwa uongozi na kusahau yakuwa bosi ni mfanyakazi wake yeye katika kufuata yale atakayo ili atimize ndoto zake yule msanii husika.

Na msanii ukiwa mwenye kujua maana ya utendaji kati yako wewe na uongozi ni wazi nyakati zote watakuwa begani kwako.

Kuna semi ya mswahili yasema “Milima ya mbali haina mawe”

Tafakari..!!!

 

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa