Kivuko atumiacho Aslay kuwavuka wasanii wengi ni uandishi.

Kivuko atumiacho Aslay kuwavuka wasanii wengi ni uandishi.

Ni wazi ukitaja listi ya wasanii ambao wameweza kuirudisha ile bongo fleva yenyewe ni Aslay. Bongo fleva ilijaa uandishi mzuri mno tangu kuchipua kwake,lakini miaka mitatu nyuma tumeona namna ya upepo mbaya wa Nigeria Fleva na South zikitawala zaidi na wasanii kusimamia hapo huku wakiamini yakuwa ndiyo muziki pendwa na muziki ambao unauza.

Kiukweli yapasa tumpongeze Aslay kwa kubadilisha nyekundu kuwa njano. Tangu aanze kufanya kazi kama msanii ambaye anajitegemea katika muda mfupi ameweza kutoa ngoma nyingi kwa wakati mfupi.

Na wapo ambao wanasema ameweza tamba maana anatoa ngoma nyingi kwa wakati mmoja. Kwa hakika yapasa tuwashangae wasemayo hayo kwa maana kama anegetoa nyimbo zenye ladha mbaya na ladha ya Nigeria ni wazi asingeweza kupata soko mbele ya mashabiki wa sasa ambao wanafuatilia muziki wa huko Nigeria kuliko hata wanahabari na wasanii.

Lakini katika mambo ambayo yalikosekana katika muziki huu ni uandishi hivyo mashabiki walichoka na uandishi mwepesi ambao inaonyesha namna ya msanii kutokufikiri kwa maana ya zile nyimbo ambazo wenyewe huita mizuka tu kwa maana ya tulikiwa studio.

Ni wazi inaonyesha namna ya Aslay alivyosoma mchezo na kuona yapasa awekeze kwenye uandishi ila aweze kuchukua soko lake. Na twaambieni sasa mtasikia nyimbo nyingi zenye uandishi mzuri kwa wasanii kuiga mfano mwema wa Aslay.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa