Kipi mnashangazwa nacho juu ya Whozu kusajiliwa Tigo Fiesta

Kipi mnashangazwa nacho juu ya Whozu kusajiliwa Tigo Fiesta?.

Msimu wa Tigo Fiesta ni jana umetangazwa rasmi katika mwanzo wake. Na hakika katika kila kijiwe cha muziki habari ya sasa ni Tigo Fiesta. (Uhalisi)

Ila shangazo kuu ni namna ya mashangazo ya watu katika upana wa kutajwa Whozu kwenye listi ya mwanzo kabisa.

Maswali ni mengi mno, yakuwa ni nani? ataimba nini kwenye jukwaa?. Mbona ni mwepesi mno na ametajwa kwa uzito mkubwa?.

Ni wazi mashabiki hawakosei katika ulizo la maswali hayo. Maana ni kweli hawamjui msanii huyu, na ni uhalisi hajulikani na hana umaarufu mbele ya mashabiki wa muziki.

Bali umaarufu wake ni kwa watu maarufu zaidi hasa katika kushinda nao kila leo katika maeneo mengi ya studio na nje.

Lakini mashabiki mkumbuke yakuwa Tigo Fiesta hutoa nafasi kwa wasanii wengi wachanga na baadae kuweza kuwa wakubwa kwa ukubwa.

Ipo mifano mingi mno ya wasanii ambao walipewa nafasi katika udogo na sasa ni wakubwa.

Kwani mmesahau Baraka Da Prince, Jux, Nandy, Billnass, Mwasiti, Linah,Vannesa Mdee, Diamond, Nikki wa Pili na wengine wengi. Ikumbukwe nao walipewa nafasi kama ambayo amepewa Whozu sasa.

Kikubwa ni Whozu kutumia nafasi vyema kwa maana macho ya wote yapo kwenye jukwaa Fiesta sasa. Hivyo atumie muda huu kwa nguvu zake zote na upana wa kipawa chake.

#TuzungumzeMuziki