Kipaji pekee hakitoshi kwa Stopa bali muongozo wa mtu mwenye ujuzi wa biashara.

Kipaji pekee hakitoshi kwa Stopa bali muongozo wa mtu mwenye ujuzi wa biashara.

Nyakati zote kwa waswahili ni hekima kunena yenye kweli juu ya yenye neema katika maisha mmoja na mwingine.

“Kweli yenye maana ni ile yenye kunenwa hadharani, lakini kweli mbaya ni ile ya ukimya” ambayo kiupana haina maana kwa kuwa indani mwako.

Na semi ya mswahili yanena ‘Lenye kufaa kueeleza, lieleze lisilofaa limeze” Hakika la msanii wa hiphop Stopa lafaa kulieleza.

Stopa ni msanii wa hiphop mwenye ujazo tosha kwa msanii bora, kwa upana wa uandishi, midondoko, kucheza na maneno, pamoja na kujiamini.

Style tatu ni wimbo wake ambao ni alama bora ya nyakati zote kuwa yeye ni mpana katika kubadili midondoko lakini namna ya  kucheza na maneno katika ladha tofauti kwenye wimbo mmoja.

Hiki ni kitu adimu kabisa kwa wasanii wengi, maana wengi tuwasikiao ni wenye midondoko kana kwamba wanatusomea hadithi kuanzia wimbo mmoja mpaka mwingine. “Uhalisi”. Lakini ndiyo tuaminishwao kuwa ni bora nyakati zote. ‘Fedheha”

Kuna ugumu mkubwa kwa msanii wa hiphop kufanya kazi na meneja au msimamizi wa kazi zake mwenye ujuzi wa biashara, lakini hii ni katika muziki wetu hapa Tanzania tu.

Kufanya yote kwa nyakati moja kumemfanya Stopa kukwama kimuziki, ni wazi hawezi kufanya yote yani muziki na kujisimamia katika mlengo wa biashara kwa ukubwa.

Kwa ukubwa wa kipaji yafaa apate mjuzi wa biashara na yeye abaki kufanya kazi ya uzalishaji bidhaa tu, soko la mauzo na matangazo yabaki kwa mjuzi wa biashara.

Ni wazi pekee hatoshi kabisa lakini atosha katika uzalishaji wa bidhaa yake ya muziki, na mswahili hunena yakuwa “Figa moja haliinjiki chungu”. Tafakari…

#TuzungumzeMuziki