Kilichomkuta Stamina kitawakuta wasanii wengi

t7035

Kilichomkuta Stamina kitawakuta wasanii wengi

Ilikuwa ni tarehe 21/1/2016 pale ambapo msanii wa hiphop Stamina alipoamua kuingiza album yake sokoni. Ambapo pia kabla ya kwenda sokoni team tizneez ilimpatia andiko la kueleza vile ambavyo album hiyo itakuwa ikipatikana.

Hakika nilikuwa mmoja kati ya wengi waliosifu uamuzi wa Stamina kutoa album, maana ni wazi katika muziki wa kizazi kipya ni kitu tunachokosa sasa. Na wasanii wengi wanaochipukia wameendelea kubaki chipukizi kwa kukosa album.

Sina mwingine wa kumlaumu zaidi ya msanii husika ambaye ni wazi akili yake inashikwa na kituo cha radio chenye kuaminisha wasanii kuwa album haiuzi. Lakini papo hapo wasanii wa dini, taarabu, bolingo hata nyimbo za asili wameendelea kunufaika na mauzo ya album. Ila hawa watu wa media hawafanyi kwenye album tu bali hata kuwapangia wasanii cha kuimba, maana ni wazi wanataka uwe vile wanavyotaka wao. Lakini pia ikumbukwe kama unampangia mtu cha kuimba ni wazi unaweka mipaka katika kazi yake ya ubunifu.

Sioni tabu kushika kalamu yangu na kuandika maandiko ambayo ni wazi ni msaada kwa wasanii wajao na hata waliopo katika kukuza sanaa zao na hata kujenga heshima inayostahili.

Yamkini wapo wengi wasiofahamu maana halisi ya Album katika muziki. Album katika muziki ni mkusanyiko wa nyimbo fulani ambazo zinakuwa zinapatikana/kuhifadhiwa kwa pamoja. Katika album ya muziki tunaona wazi mara nyingi kuna kuwa na nyimbo nyingi ambazo haziruhusiwi kuchezwa katika vituo vya radio. Isipokuwa kutakuwa na nyimbo tatu au mbili ambazo ni wazi huachiwa ili kusaidia mauzo yani kutambulisha album ya msanii husika. Hivyo kama una nunua album ya msanii fulani ni wazi utakuta nyimbo nyingi zikiwa hazijawahi kusikika mahala popote zaidi kwenye album husika

Wasanii wengi walioibuka kuanzia 2010 ni wasanii wazuri wenye vipaji vya hali ya juu. Ila wengi wao wametawaliwa kifikra sio wasanii wenye fikra pevu, hasa katika kujenga heshima zao katika nyakati zijazo.”Tengeneza kesho yako”

“Majuto ni mjukuu”si jambo la kuficha maana watu tunajifunza kwa watu waliokosea ili tusikosee katika sehemu ile. Ni wazi ukitizama makosa katika mkusanyiko wa nyimbo za Stamina ambazo ameziweka katika kitu kimoja na kujaribu kusema kama ni album. Yaweza kuwa tuna mitazamo tofauti katika kujua maana halisi ya album. Lakini ni wazi huwezi sema msanii anatoa album ya nyimbo 15 na kati ya nyimbo 15 ni nyimbo 5 kama sio 4 ambazo huvijawahi kuzisikia katika vituo vya radio.

Hakika hili limefanya hata mwenyewe Stamina kukosa hata nguvu ya kusukuma huu mkusanyiko wa nyimbo zake katika mitadao ya kijamii. Na hata kufuta zile post chache na za kinyonge juu ya kusanyo la nyimbo zake 15 tu. Kiuhalisia ni jambo la kusikitisha kama leo msanii kama Stamina anakosa kuwa na album, maana ni moja kati ya wasanii wachache wenye tungo nzuri na flow zenye kusikika vyema.

Lakini jambo hili hakika linakwenda kuwakuta wasanii walio wengi, na inaweza kuwa wakaua wenyewe soko la album na yale wanayosema album haiuzi yakawa yametimia.

Leo kuna wasanii wengi tumekuwa nimekuwa nikiwasikia wakifanya vyema na wamekuwa na nyimbo nyingi ambapo kiuhalisia walipaswa kuwa na album, lakini wamekubali kuendelea kuwa chipukizi kwa kukosa album. Wengi wamekuwa wakiamini kauli zisizo na tija zenye kutajwa bila hata kumeza mate na watu wa media yakuwa album haiuzi. Ikumbukwe pia “Mbio za sakafuni huishia ukingoni”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez