Kila msanii na Record Label, Je wanajua maana, na uendeshaji wake?

images

Kila msanii na Record Label, Je wanajua maana, na uendeshaji wake?

Tumeona kila msanii akihojiwa kwenye vyombo vya habari husema nafungua Record Label yangu, lakini kiuhalisia wengi wao hawajui maana wala uendeshaji wa Label hizo.Isipokuwa ni kwenda na kasi ya upepo.

Record Label: ni Kampuni ambazo zinasimamia kazi za msanii au wasanii kwenye uzalishaji, Utangazaji, usambazaji na mauzo ya kazi zao. Lakini katika Label huwa kuna label kubwa yani (Major Labels) na pia kuna Label ndogo (Indie/Independent Labels)

Major Label ni zile ambazo zina milikiwa na major corporation Kama Sony, na Universal, na hao husimamia bajeti nzima ya msanii kuanzia gharama za kurekodi nyimbo, gharama za malazi, chakula (allowance), promotion ya kazi, manufacture, na distribution. Hela Yao inakuja kurudi kwenye mauzo ya kazi hizo (CD sales) hivyo mkataba wao na msanii unakuwa ni wa kumgharamia msanii kazi zake na ikitoka kinachopatikana kwanza wanatoa walichotumia halafu kinachobaki wanagawana asimilia walizokubaliana na msanii husika.

Katika mfumo huo, msanii anakuwa huru kujipatia kipato kwenye kufanya matumbuizo na kuuza bidhaa za brand yake (merchandise) bila kuingiliwa (no interference) na record label yake. Ila Baada ya mauzo ya Album kuanza kushuka, Record Label zikaanzisha kitu kinaitwa “360 record deal”  ambazo zenyewe sasa zikawa zina mgharamia msanii kila kitu na kuchukua pato lao la mauzo ya CD Ila pia wakaanza kuchukua na pato la mauzo ya tikiti za tumbuizo , na merchandise mfano ukitoa tshirt zako na wao wanapata asilimia maana wao ndio wameijenga hiyo brand. Katika mfumo huu Sasa Maana wanaingilia mauzo yako, ndio ikafanya wawe na wajibu wa kuhusika na kuhakikisha wanakutafutia matumbuizo wenyewe.

Hivyo basi msanii aliyesainiwa na major label no almost guaranteed kufanya tours na show nyingi Kwa Mwaka Maana mabosi wake ndio wanapanga kazi.

Indie/Independent Label, Hizi ni labels ambazo zilianzishwa na Watu binafsi Bila kuwa na bajeti kubwa Maana hawana support ya corporations kubwa, Ila zimekuwa zikifanya kazi Kama jinsi record commonly kubwa zikifanya. Pia record label hizi Ndogo bado Kwa kiasi flani zimekuwa zikiingia ubia na Record Label kubwa inapokuja kwenye swala la distribution pale CD ya msanii wao inapokuwa tayari kutoka. ( Maana zoezi la kuhakikisha CD kupatikana Kila duka dunia nzima asubuhi ya release date sio kazi rahisi Kwa independent label)

Mara nyingi label hizo huanzishwa na wasanii wenyewe au watu wao wa karibu ambao wana hela kidogo ya ku invest kwenye sanaa zao. Na mode yao ya uendeshaji kazi ni DIY ikimaanisha “Do It Yourself” na pia “the more you invest, the more you get out of your investment”. So unachokipata chote kinarudi kwako na unaogawana nao ni wale ambao umesaidiana nao kuanzisha au kuinvest kwenye kazi yako na sio kampuni kubwa
Major Labels duniani zipo 4 tu zinaitwa “the Big 4” ambazo zenyewe zina vi label vingi chini yake, so whether umesign direct kwao Au Kwa label zake ambazo imezitenga mahususi kukidhi kila aina ya muziki flani specifically, bado upo kwenye major label. Sony Music Group (Columbia Records, Jive Records, Epic Records, Universal Music Group (Interscope Records, Def Jam Records, Geffen Records, Island Records, Roc A Fella Records, So So Def Records) EMI (EMI Music, Capitol Records) Warner Music Group ( Elektra Records, Atlantic Records, na Badboy Records)

Independent labels zipo nyingi ambazo either ni za wasanii, Au ni za washikaji wafanyabiashara. Nyingi zinafanya kazi chini ya Labels zinazomilikiwa na “The Big Four” na baadhi zinafanya zenyewe tu Kama zenyewe na inawezekana zikisaidiwa na Big 4 Kwa makubaliano kwenye Suala la distribution. Mfano wa Label hizo ni Cash Money Records, Young Money Records, G Unit Record, MMG, Grand Hustle,Taylor Gang, TDE, No Limit Records,Blackwall Street, Good Music, Shady Records, Aftermath Recordsa na nyingine nyingi.

Na katika mfumo wa Label msanii anaweza kuwa chini ya Label fulani na yeye akaanzisha Label yake. Mfano ni kama Dr Dre alikuwa signed na Interscope records (Major Label).  Akaanzisha label yake Aftermath, ikawa chini ya Interscope. Akamchukua Eminem akam sign Aftermath, so automatically akawa signed Interscope pia.

Kuna mifano mingi katika upana a Records Label. Ila katika Label zetu ambazo wasanii wetu wamekuwa wakipaza sauti zao kuwa nina Records Label ni vyema kukaa na kutafakari zaidi.

Je ni wamefika vigezo vya kusema anamiliki/wanamiliki Records Label? Au wapo kwa kufuata upepo kama bendera? Tunaona sasa hata mtu akiweza kumlipia msanii kurekodi wimbo mmoja na kumposti Instagram nae anasema ana Record Label. Ni vyema kujifunza kwanza ili tuweze kufika mbali, najua hakuna kinachoshindikana kama kweli kutakuwa na muda wa kujifunza zaidi.

Hii ndio maana na undeshwaji wa Records Label.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez