Kila msanii atakaye fuata mbio za Diamond Platnumz atafanikiwa. (Muziki)

Kila msanii atakaye fuata mbio za Diamond Platnumz atafanikiwa. (Muziki)

Ni juzi katika siku iliyokuu ya Eid ambapo Diamond Platnumz pekee ameweza kujaza uwanja wa mpira. (Kahama)

Na katika uhalisi kwa mujibu wa wajuzi wanatujuza yakuwa anakuwa ni msanii wa kwanza pekee Tanzania kuwahi kujaza uwanja. (Naam)

Ikumbukwe wengi hujaza wakiwa na listi ya wasanii wengi zaidi, lakini Diamond Platnumz amejaza pekee. (Kabisa)

Na daima waswahili hunena yakuwa “Mwenye sifa yake mpe” sisi ni nani kiasi tusisifu upana wa Diamond katika jazo la uwanja? (Shangazo)

Ni wazi jambo la kumpongeza mno, na kupitia tamasha lile ni wazi amepandisha thamani kubwa muziki huu. (Ndiyo)

Ameonyesha nguvu yake lakini nguvu ya bongo fleva katika upana wake. Kwanini asipongezwe? (Pongezi)

Na kama wasanii watafuata mbio za Diamond katika muziki hakika watafanikiwa vyema. Maana yapasa “Tuige yenye maana, si yasiyo na maana” (Uhalisia)

Na shoo imekuwa bora kwa namna ya maandalizi yake namna ya matangazo, lakini matumizi ya bendi kadhalika jinsi alivyoweza kutumbuiza Diamond Platnumz. (Ubunifu)

Jambo jema ni namna alikuwa ametulia bila mapepe kama ambavyo tumezoea katika matumbuizo yake mengi. (Eeh)

Kukaa jukwaani zaidi ya saa 5 si jambo dogo huku upana wa kuimba na kucheza ukiwa ni katika ujazo ule ule. (Ukomavu)

Na ambacho tunapenda kusema ni wazi Diamond ni msanii kamili mwenye ukamili. Ni vyema pia akajua yakuwa “Ushindane na mtu ikiwa hakudhuru kwa lolote” ( Mfalme)

#MuzikiNiSisi