KIKAO CHA WASANII CHA KISANII Sehemu ya II

SennMicrophone

Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa siku nyingine amani na utulivu katika nchi yangu,Huku wengi wapenda maendeleo tukifurahi kwa ushindi wa Mbwata Samatta kwa kutunyanyua watanzania baada ya kuwa mchezaji bora Afrika anayecheza ligi ya ndani.Hii haijagusa wapenda soka peke yao hii imegusa watu wa kila namna.Team tizneez inakupongeza tena Samatta kwa tuzo hiyo yenye heshma kwa nchi yetu.

Swala la mirabaha limeonekana kuteka hisia za wasanii pamoja na mashabiki walio wengi,Kiukweli ni jambo jema na zuri kuona watu wanaamka na kudai haki zao.Wasanii wetu wanafanya kazi nzuri na zakuvutia.Muda huu ninapoafanya majukumu yangu nimekuwa nikisiliza zaidi wimbo wa msanii Jay Mo unaoitwa hili game uliotoka mwishoni mwa mwaka 2015.
Kweli hili game tough, maana lina mambo mengi ya kurekebisha kwanza tuanze kwa kutoa maslahi binafsi.Maana wapo walio karibu na wadau ambao kwa kunyenyekea kwao kunafanya watumiwe kubadilisha misimamo ya wengine wenye kutambua haki zao.
Kwa mtazamo tu  chama cha wasanii (TUMA)kianze kwa kutoa elimu juu ya malipo ya mirabaha. Maana katika andiko la kwanza ambapo Tizneez ilihoji uhalili wa kikao kilichofanyika THT cha baadhi ya wasanii ambacho hakikuwa na ushirikishwaji wa wasanii walio wengi. Nikki wa Pili alisema “Kikao cha THT kilikuwa ni cha kujitolea kueleimisha hakina uhusiano wowote na kikao cha Protea hotel USIPOTOSHE”

kuji                                                       Picha kuonyesha Tweet ya Nikki wa pili
Sasa kama ni kikao cha kueleimisha si ilibidi kitangazwe zaidi ili wasanii wengi wajitokeze wapate hiyo elimu?.Kwenye hili wala halihitaji elimu ya juu kuchambua hata sisi wa darasa la saba tunaweza kupembua na kupata majibu mazuri.
Turudi lengo kuu katika muendelezo huu wa wasanii na kikao cha kisanii.Hapa kuna wengi ambao hawajui wanachokipigania ila kuna wachache watanufaika na kile kinachoendelea sasa. Yani kutokuwa na imani na CMEA, Kuvunjwa kwa bodi ya COSOTA na media kuendelea kupiga nyimbo zao bure.
Ngoja tuwekane sawa kwanza kabla ya kuendelea mbele zaidi, CMEA na COSOTA katika semina iliyofanyika pale Sayansi Kijito nyama mwishoni mwaka huu walitoa fursa ya wasanii kuuliza maswali na wengine kuzungumza mitazamo yao.Ila wapo wasanii kadhaa waliozungumza kwa niaba ya wengine,ilikuwa si rahisi wote kuzungumza pale. Waliouliza maswali walipata majibu kutoka kwa  CMEA  na COSOTA
Na hakuna aliyepinga majipu yalitolewa. Kwa maana nijuavyo kama hujaridhika na majipu ya swali lako si unasema? Lakini naamini kila msanii alilidhishwa na majibu yale na hata baada ya kikao wakapata chakula cha pamoja na hata kupiga picha za pamoja kama ishara ya kupongezana.
Siandiki kukatisha tamaa wasanii ila naandika kuhusu kumkomboa msanii. Hivi unaweza kujifungia ndani na jambazi harafu ukaanza kueleza jinsi utakavyojilinda usiku? aaah huu ni mfano tu ambao hata hauhusiani na mziki.
Wazee wetu husema mjinga na mpumbavu wote hupotea pamoja. Maana yangu nini hapa unaweza kuona CMEA imepingwa kwa nguvu zote halafu baadae inatokea anakabidhiwa mtu mwingine lakini huyu mtu kawekwa tu na wenye uwezo. Tafadhali ndugu zangu msije mkatumia ule msemo wa zamani wa wazee wetu “mchawi mpe mwanao akulele”. Misemo mingine haikuwa na maana.
Kuna mingi mitazamo iliyotokea jana katikaTwitter,Instagram na group la ‘Wasanii Tz’ kwenye WhatsApp. Ngoja tuweke sawa tena kabla ya kwenda mbele
Gnako aliandika  “Aliyeandika hiyo makala na aliyemtuma hawawezi kushindana wala kuwa na mtazamo wetu kwanza ndo kazi imeanza tusonge”

Kwanza kabisa naomba kuweka wazi juu ya swala alilozungumzia GNako kwamba nimetumwa. Ukweli ni kwamba sijatumwa na mtu yoyote na kama yupo ajitokeze adharani. Lakini pia kauli ya huyu bwana inanipa mashaka ni jinsi gani hawa jamaa (GNako) ambavyo aelewi anachokizungumza, Jiulize swali dogo tu, kuna mtu ambaye anafanya biashara bila kutarajia faida. Lakini katika tafakari yangu nikagundua huenda hawa mabwana na kigenge chao wanampango wa kuanzisha NGO ya mziki, ambayo kazi yake itakuwa ni kuburudisha jamii ya Watanzania bure. Ni jambo jema kama wameamua kufanya hivyo na kwa hakika wanastahili pongezi za dhati kabisa tukianzia kwa kiongozi wao na mpaka kwa mfuasi wa mwisho. Lakini kama huyu jamaa anafanya biashara ananitia wasiwasi kidogo.
Hapa naendelea kupata mashaka zaidi hivi kwani wasanii wanapambana na nani katika hili swala la mirabaha? Isije ikawa hawajui mtu wanaepambana naye.
Bill Nass “Waandishi wengi wa makala kazi yao kuu ni kuonesha umahiri wao katika kukosoa na kuchanganua miono yao,kuonesha tu kipaji chao na sio kujenga,mpeni hongera aliyeandika makala hii kuwa ana kipaji ila haturudi nyuma ng’oo”
Asante sana Bill kwa kutambua kipaji changu! lakini naomba nikurudishie swali, Je ni yupi anatambua uchungu na shida ya mwiba kati ya aliyeota tende au aliyechomwa na mwiba siku ya kwanza? Usijiite mpambanaji kwamana kuna watu wanaudai mziki pesa nyingi na wamenyamaza kimya ilihali wanajua kile kinachoendelea. Ndipo tunaporudi palepale Kelele za mlango azimzuii mwenye nyumba kupata usingizi. Hapa napata mashaka tena na tena hivi ni kweli wasanii wote wanajua wanachopigania sasa? Hii ni kasumba ya walio wengi yani hata kama kafanya kitu kibaya anataka umsifie. Ni watu makini na wachache ambao ukikosea watasema umekosea.Kweli wasanii kusema kazi zao ziendele kuchezwa bure kwenye media hii nayo tunatakiwa waandishi tusifie?
Snura Mushi “Kiukwel me nimeisoma ila nakumbuka nick alisema hii ni vita na kwenye vita kila upande unahitaji ushindi,na kila mtu ana mbinu zake msishangae mkagombanishwa na kukatishwa tamaa hayo mambo ndo yameanza na yakakuja mengi kama hay oau zaidi ya hayo.Kikubwa ni msimamo wetu wetu tusikubali kuyumbiswa na wote tuwe kitu kimoja kama tulivyoaamua kuwa pamoja kwenye kikao naiwe hivyo wapo watakao kutoa akili,watakaosema hatujiamini nk,cha msingi nikujua hii ni vita na yaweza kuwa tunaopambananao wengine hatuwajui acha watuone wapumbavu leo kesho watatuelewa.” Snura alisema hayo baada ya Ruta Bushoke kutuma link iliyobeba makala hiyo. Snura ananikumbusha msemo ambao mara nyingi nimekuwa nikusikia wa “Kikulacho kinguoni mwako” Big G walioonjeshwa ama kwa hakika haitadumu kuwa na utamu. Je amefikiria hivyo? au asiyejua maana tusimwambie maana?

Lakini pia nina mashaka kwa nini Nikki aliamua kutangaza vita? kama ambavyo snura amesema katika ujumbe wake? Hivi ni kweli mtu analazimishwa kupewa haki yake? Inamana Snura hapendi pesa?
Chungeni katika hili maana anayewayumbisha yaweza mpo nae na anatumia nguvu ndogo kuwagawa ili mshindwe kuapata haki yenu.
Lengo ni kujenga sio kutengeneza mfumo wenye kunufaisha wachache kila iitwapo leo. Wasanii na kikao cha wasanii.leo tuishie hapa tutaendelea.

Bonyeza hapa kusoma sehemu ya kwanza ya WASANII NA KIKAO CHA KISANII
Cc# www.tizneez.com

Instagram@tizneez
Twitter@tizneez
Facebook@tizneez