Kifungo cha Nandy ufunguo wake ni ‘kuidharau aibu

Kifungo cha Nandy ufunguo wake ni ‘kuidharau aibu’

Twaipaza sauti katika hekima na ufahamu na hasa sikio la Nandy lapaswa kusikia vyema ilihali apate ufahamu katika andiko hili jema.

Hakika chukizo letu ni kubwa katika mlengo wa kufadhaishwa kila leo kwa msanii Nandy hasa katika tukio baya lililotokea wiki chache nyuma.

Tukio lilihusisha kusambaa kwa video yake ya faragha akiwa na msanii mwenzake Billnass.

Katika uhalisia katika kuta nne kwa maana ya chumba, kuna mengi mno. Isipokuwa ni kwa kuwa yetu hayajawa wazi tu, na yote ni katika muda.

Licha ya fedheha hii, lakini Nandy alikubali mbele ya hadhara na ni katika kuomba radhi.

Hakika kwa waungwana na mwenye ufahamu radhi ni jambo lenye kuheshimiwa mno, bali wenye hovyo si kitu.

Nguvu itumikayo katika Blog nyingi na kurasa nyingi kubwa za mitandao ya kijamii husasani ‘instagram’ ni katika endelezo la kumfadhaisha Nandy.

Jambo hili si jema kwa maana haipaswi kusimamia yaliyo mabaya yenye kujaza maumivu katika moyo wa mtu bali yenye faraja juu yake.

Na chukizo letu ni kwa mashabiki wengi kuonekana ni wenye kufurahia zaidi, hii inatupa taswira ya yakuwa tupo katika kizazi cha hovyo zaidi ambacho kinapendezwa na fedheha ya mtu na si kazi. (Soni)

Lakini daima mswahili hunena yakuwa “Usigombane na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi” (Ufahamu) Tafakari.

Hakika yampasa Nandy awe jasiri katika fedheha nyingi za sasa maana maandiko mema yanena “Busara itakulinda ilihali hekima itakuhifadhi”

‘Idharau aibu’ na upate uisho wa furaha nyakati zote. Hakika ‘Kuidharau aibu’ ni funguo njema, wala hapaswi kulia wala kujawa na unyonge bali ‘Idharau aibu’

#TuzungumzeMuziki