KIFO CHA SINGELI KIMEWADIA CHINI YA MIKONO YA MAHARAMIA

IMG_20160927_225651
Kuna Kitu sikipendi sana nacho ni kuigana tena kuigana kwa nia ya kuharibiana au kupoteza uhalisia wa unachokiiga Ili mkose wote, wakati radio ya E.FM 93.7 inaanza kurusha matangazo yake walitafuta njia zao za kupata wasikilizaji na moja ya njia kuu walizotumia ni kucheza aina za muziki ambazo zinapendwa sana na jamii ya watu wa uswahilini au uswazi. Muziki huo ni kama Mnanda na Singeli,kwa Poa muda mfupi waliweza kupata wasikilizaji na radio yao ikawa juu na hata walipoanzisha vipindi vyao waliendelea na utaratibu huo wa kucheza Mnanda na Singeli na hadi Leo upo na kupelekea kufanyika kwa matamasha makubwa ya Singeli, Lakini wakati wanaanza baaadhi ya watu waliitazama radio hiyo kama ya kihuni na haitapata nafasi kubwa na hata baadhi ya radio zingine zikiwaponda. Kilichonifanya nitoe dukuduku langu Katika hili ni baada ya kusikia Radio Nyingine wakiinadi Singeli kuipeleka kimataifa pamoja na kuanzisha mashindano ya Singeli na maneno mengi ambayo kwa kweli kwa upande wangu naona ni kuishiwa mawazo na mipango Kwani huko ni kuiga kwa uwazi kabisa,mlikua wapi wakati wenzenu wanabuni kitu chao??? Aina ngapi za muziki mshazipeleka kimataifa?? Wasanii wangapi wanawalalamikia mnawaua vipaji vyao?? Mngetafuta aina nyingine za muziki ambazo hazipewi nafasi ili muanze nazo. Nawasikitikia sana wasanii wa Singeli Kwani kwa sasa hawajui washike wapi lakini wakumbuke nani aliewafanya wakawa hapo walipo na muziki wao ukawa juu. Naona sasa tabia ya kuigana kwenye vipindi na utangazaji inahama Sasa mnaelekea kwenye kuibiana mawazo na mipango. Wengi wamekua kimya katika hili lakini mimi kama msanii na pia sipendi mambo ya kijinga kama Haya niliweka nadhiri nitaongea na leo nimetimiza nadhiri yangu. Tusiwe tunaangalia nani kafanya ndio tuseme tuangalie yeyote anaekosea Ili arekebishwe.

BY: NASH MC