‘Kichwa kisicho na akili ni adhabu kwa miguu’ “Young Dee”

‘Kichwa kisicho na akili ni adhabu kwa miguu’ “Young Dee”

Kusema yenye kweli ile ya muziki kwenye mambo ya kiki  haiwezi kuja kuwa na mwisho kwetu sisi hata mara moja, bali pale kiki zitakapokuwa zimezimwa na kuwashwa muziki. #ZimaKikiWashaMuziki.

Ilihali wapo ambao wanasema tuache kuandika hawa wafanya kiki maana tukiandika ni wazi tunawapa nafasi na hilo ndiyo huwa lengo lao. Hivyo tunakuwa daraja jema la kuwavusha juu ya chombo chao cha kiki.

Lakini ndugu zetu yapasa tufahamu “Mwindaji hawezi kupumzika, ila baada ya kupika”

Ama!kweli! “Mzoea vya kunyonga vya kuchinja hawezi” Ni wazi sasa Young Dee ameingia katika kundi baya la wasanii wapenda kiki. Lakini imefika mahala yatupasa tushishangae haya kwa maana “Kama theluji wakati wa mvua, na mvua wakati wa mavuno kadhalika heshima haimpasi mpumbavu” lakini “Kama mbwa arudiavyo matapishi yake, kadharika mpumbavu kurudia upumbavu wake”

Akili ya ubunifu wa muziki imekwisha potea kwa Young Dee, akili pekee iliyobaki ni akili ya kutaka mambo ya kiki. Hofu yetu sisi ni kuwa “Usipoumiza akili utaumiza mwili”

Ya nini tusiambiane ukweli? Hapana! Young dee ameonekana kusahau muda mchache tu amefanya vyema na wimbo wake wa Bongo Bahati Mbaya bila kufanya kiki ya aina yoyote ile.

Inashagaza katika muda huu kusambaa kwa picha zisizofaa kati yake na Amber Lulu, huku Young akiwa mwepesi kuandika picha hizo zilikuwa kwaajili ya mavazi mapya hivyo anaomba ladhi kwa kuvuja kwa picha hizo bila ya idhini yake” Ila “Fumbo mfumbie mjinga mwerevu huligandua”

Katika akili ya kawaida alikuwa ladhi kupiga picha hizo sasa kipi ambacho kinamshangaza kusambaa kwa picha hizo? Au wakati anapiga alitegemea nini kitatokea? Ama kweli! “Hakuna shule ya akili”

“Asali na shurubat haina ladha moja” Ni wazi anguko la kimuziki laweza mfika kijana huyu kama tu asipotaka kuumiza akili kwenye akili ya Sanaa na kuegemea kwenye akili ya mwili kwa namna ya kiki.

Ni vyema kujitafakari vyema kwa maana ya kujenga mashabiki ambao watafutalia zaidi muziki wake si mambo ya kiki. Kwa maana ya “Kizuri chajiuza na kibaya cha jitembeza”

#ZimaKikiWashaMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa