Kichwa kisicho na akili ni adhabu kwa miguu (Rose Ree)

Kichwa kisicho na akili ni adhabu kwa miguu (Rose Ree)

Neno muziki biashara na biashara ya muziki limekuwa likiyumbisha mno wasanii wa kizazi hiki.

Wengi hawaelewi maana ya muziki biashara wala biashara ya muziki. Bali kasi ya neno kuwazidi katika matendo ya nje ya muziki na sio muziki wenyewe. (Ujinga)

Tusiposema sisi ukweli huu aseme nani? Ni wazi hakuna maana wengi hupenda Zaidi kusifu visivyo na maana. (Fedheha)

Hatuwezi kuacha kusema Rosa Ree ni moja kati ya marapa bora wa kike ambao wametokea kuwepo katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Lakini ndugu zetu mwapasa kuzingatia yakuwa “Hakuna shule ya akili” lakini yapasa mjue “Shati bovu si mgongo wazi” (Akili).

Na bila kumuweka katika njia sahihi ya kusimamia muziki wake ni wazi atapita kiwepese kama pepo za bahari ya hindi au kama mtu afunguapo taulo wakati yu msalani.

Kasi ya Rose kuweka mwili wake wazi ni kubwa mno, na mwenyewe huona ni vyema maana ameona ni mwenye kuonekana katika kurasa nyingi zenye watu wengi Zaidi. (Udaku)

Lakini anapaswa kujua Je! kurasa hizo zina maana kwenye muziki wake? Ni wazi hazina maana katika ile kweli mashabiki watamuhamisha kutoka kwenye Sanaa na kumuweka kwenye kundi la wale wadada waweka miili wazi kwenye mitandao. (Gigy Money)

Bila kificho muziki wetu haujafika hatua za kuishi kama aishivyo Rosa ree kwenye mitandao ya kijamii.

Hivyo ambao wanahubiri yakuwa yuko sawa ni wazi si wenye kumtakia mema bali kumuelekeza shimoni.

Lakini hatupaswi kufedheka juu yake maana waswahili husema “Mwenye hekima huogopa na akajitenga na uovu bali mpumbavu ana ufidhuli na kujitumai”

Na daima waswahili husema “Usipotaka kuumiza akili utaumiza mwili” Ni vyema Rose asimame vyema kwenye muziki kwa maana kuumiza akili katika biashara ya muziki na si kutangaza mwili wake Zaidi bali muziki.

Tafakar…!

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa