“Kiburi ndicho kinachowaangamiza wasanii”

“Kiburi ndicho kinachowaangamiza wasanii”

“Msema kweli hana wajoli” na ni wazi hatuna chembe ya wajoli mbele ya kusema ile kweli yenye kweli wakati wote.

Lakini yapasa jamii ijue “mshale usio na nyoya hauendi mbali” hivyo bila ya kuvua viburi ni wazi wasanii wetu hawatafika mbali kwenye mafanikio ya kazi zao.

Daima haki/faida haikufuati bali kuitafuta popote ilipo, katika ile bahati ya mtende waliyonayo wasanii wengi wa sasa ni viongozi wa kiserikali kuwafuata wao na kutaka kujadili namna ya kupata manufaa juu ya kazi zao.

Ila ni wazi miaka ya zamani haikuwa ni rahisi kwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia muziki kuwa karibu na wasanii kama ambavyo sasa imekuwa hivyo.

Bahati hii ya wazi wasanii wameshindwa kuitumia vyema kwa maana ya kujitokeza kwa uchache mkubwa mno. Ni wazi viburi vimetawala katika mioyo yao.

Hakika hii ni aibu kubwa, na katika uwazi wao ndiyo wahanga wakuu wa jambo hili kuliko waziri husika. Lakini wasanii hawa ni wepesi mno katika kukutana kwenye vijiwe vya pombe na vijiwe vya usengenyaji mzuri, na miguu yao kwenda kwenye mambo ya msingi ni mizito mno bali kwenye upuuzi kuwa miyepesi.

Nafasi ambayo wameipoteza leo ni nafasi kubwa na hatupaswi kuacha kukemea vitendo vya aina hii vya wasanii kudharau mambo ya msingi. Licha ya nafasi hii huenda ikajirudia tena katika mwezi mmoja ujao. Lakini je!watajitokeza kwa wingi?au ndiyo idadi itazidi kuwa ndogo?

Wasanii ambao wamewakilisha wasanii wenzao leo/Jana ni wachache kupita kiasi. Na daima “Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” . Lakini wapo wasanii wachache ambao wamechagulia katika mambo mema mazuri yaliyopangwa kufanywa na serikali kwa upande wa wasanii, haitatushangaza kwa wasanii ambao hawajaudhuria kusema wasanii chaguliwa ni wasanii pendelewa ilihali wasanii walalamikaji hawajatokea katika mkutano huo.

Team Tizneez inatoa pongezi kwa wasanii wote ambao wamejitokeza kwenye mkutano huu wa leo/jana.

Ni vyema wasanii wengi kuvua mioyo ya kiburi katika kujenga kesho zao zenye mafanikio ya Sanaa zao. Kwa maana “Kiburi hukaa  kichwani mwa mtu mpumbavu” lakini “Utu busara, Ujinga hasara”

#AmkaMsaniiVuaKiburi

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa