Kauli ya Omg kwa hakika imejaa uongo

Kauli ya Omg kwa hakika imejaa uongo

Tuipende kweli yenye kweli maana uongo hauwezi kutusaidia hata kwa uchache kukuza sanaa ya muziki bali fedheha tu.

Kitendo cha Omg kusema yakuwa “Sababu kubwa ya kutofanya video nyingi on time ni kwa sababu directors hawatupatii yani, yani wanashindwa kwenda na idea yetu sisi” (Planet Bongo)

Ni wazi ni uongo wenye uongo ambao haupaswi kunenwa na wasanii kama wao. (Soni)

Hivi ni wazo gani ambalo wao wanakuja nalo na waongozaji wote tulionao Tanzania washindwe kupatia? achilia mbali wa nje ya nchi, maana hakika tulionao wanajitosheleza sasa.

Ni vyema wawe wazi yakuwa huenda ni bajeti ya ufanyaji video husika, lakini si waongozaji kushindwa kufanya uhalisi wa wazo lao.

Maana wajuzi upande wa uongozaji video wananena yakuwa “Hakuna wazo ambalo linashindikana kufanya na kutoka kama lilivyo bali wasanii hushindwa kufika bajeti, hivyo jambo hutoka tofauti shauri ya bajeti”

Kwa uhalisi huo ni wazi Omg wananena uongo ambao hauna maana mbele ya wajuzi bali fedheha juu yao.

Lakini mswahili hakuacha kunena yakuwa “Mtembea peku hapendi, ila hana viatu”

#TuzungumzeMuziki