“Katikati pasiwachanganye mkasahau chanzo cha Ray C”

“Katikati pasiwachanganye mkasahau chanzo cha Ray C”

Kuundwa kwa huyu na kubomolewa huyu ni mtindo huru ambao nyakati hizi umeonekana ni mwema katika muziki huu wa kizazi kipya.

Ilihali wengi ambao wameundwa  si wenye vipaji bali kwa kuwa hakuna cha kusikiliza ni wazi ni lazima wasikike vyema kwenye uwanja mpana wa muziki ambao umejaa kila aina ya fitna.

Ni mengi ambayo yemetokea juu ya Ray C katika maisha yake ya ndani ya muziki lakini nje. Na ni furaha kwetu sisi kuona ameamka vyema na kuanza kufanya tena muziki.

Ni wazi ukubwa wa kipaji chake na mambo aliyofanyia muziki huu ni wazi wafanya wengi kutamani kuona amesimama vyema Zaidi ya hapa alipo.

Lakini jahazi la muziki lipo katikati na vijana wapya katika upande wa Media ni watu ambao wamesahau vyema chanzo cha Ray C katika muziki huu ambapo ni ukweli usiopingika yakuwa amechonga barabara katika mambo mengi ya muziki kama kushirikia matumbuizo ya nje, kuchukua tuzo nyingi za nje na mengine mengi.

Katikati ya muziki tunaona ambavyo watu wa media wakizima kabisa kuzungumza juu ya muziki wa Ray C tangu kuamka tena, lakini watu hawa wapo bize kuzungumzia Zaidi habari za mume wa Shilole ambaye kimsingi hakuna umuhimu wa kuzungumzia kwa upana ambao wao wanazungumzia.

Ni vyema kutazama chanzo hichi cha Ray C lakini si vyema kusubiri tena arudie kufanya mambo ya hovyo ndiyo awe katika vinywa vyenu siku zote ambazo atakuwa na jambo baya.

Ni muda mzuri wa kuzungumzia kurudi kwake katika muziki, kwa maana hakuna litakalo mkomboa Zaidi ya kuwa wa kweli juu ya habari zake za kurudi kimuziki. Na wakati wote waswahili husema “Jitihada, ujitiahidi”

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa