Katikati pasiwachanganye mkasahau chanzo (Adam Juma)

Katikati pasiwachanganye mkasahau chanzo (Adam Juma)

Ipo furaha kwa baadhi ya waongozaji video kuona namna ya wachache wenye pakusemea pakubwa wakipindisha na kuharibu mchango wa Adam Juma katika upande wa video za muziki wa bongo fleva.

Lakini katika kweli yenye kweli Adam Juma ni chachu ya chimbuko la waongozaji wote ambao walikuja mbele yake.

Ni wazi kwa nyakati zake alifanya kwa ukubwa, na hata sasa anafanya kwa ukubwa ilihali ni katika upana wa bajeti.

Hivyo kupindisha historia yake na kuleta dhihaka ni jambo baya zaidi.

Lakini furaha wapatayo vijana wadogo katika kufedheheshwa kwa Adam Juma ni kubwa mno, ilihali wanasahau yakuwa “Nyakati hupita”

Maana mbegu wapandayo katika kufurahia watu kufuta historia kwa nguvu ndiyo iyotayo katika akili za vizazi vijavyo.

Kwa maana hata wao zitafutwa tu, hivi wanafikiri kuhusu kesho zao?
Ni wazi kama huthamini mchango (historia) ya mtu hata yako pia haita thaminiwa tena kwenye kizazi hiki chenye kukumbuka kumbukumbu.

Lakini yote ya yote ni vyema mashabiki wa video za muziki wa bongo fleva mjue yakuwa Adam Juma ni chanzo halisi, ilihali wengi wamechanganya na katikati”

Ni wazi sisi Tizneez tunathamini na kutambua mchango wa Adam Juma katika muziki huu.

#TuzungumzeMuziki