‘Kati kati pasiwachanganye mkasahau chanzo’ Stereo Sehemu ya 1

“Kati kati pasiwachanganye mkasahau chanzo” Stereo

Wengi wamekuwa wepesi wa kusahau chanzo na wepesi wa kuzungumzia kati kati. Jambo hili hatuwezi kulifungia vinywa vyetu katika kuisema ile kweli yenye kweli yenye kuleta maana kwa kizazi hiki na hata kijacho.

Jambo la upotoshaji kwa msanii wa hiphop Stereo yakuwa ni mpya na ametambulishwa kwenye muziki na Rich Mavoko tumeona kwa namna ya vile baadhi ya wachambuzi wakizungumza hivyo.

Kwetu haitubariki hata kidogo kwa maana tunajua huo sio uhalisia, bali muandikaji kuandika bila kujua kile ambacho anakiandika.

Wachambuzi wamekuwa wengi katika upande wa muziki ilihali hawajui muziki wenyewe bali kuvutwa na upepo tu wa mtandao wa picha Instagram. (Chukizo)

Ni vyema kuandika kile ambacho unakijua Zaidi kwa maana ya haya maandiko yataishi milele. Hivyo kuandika upotoshaji ni chukizo kubwa na chukizo kubwa ni kwa wale ambao ni wachambuzi ambao wameweza kuaminika kwa ukubwa tu.

Leo team Tizneez tumeona tuweke bayana ile wazi yenye uwazi juu ya msanii Stereo yakuwa si mpya kama baadhi ya wachambuzi wanavyosema.

Stereo ni moja kati ya wasanii bora kabisa wa hiphop katika uwanja wa hiphop ambaye sasa inaonekana yupo chini ya Label ya Wasafi.

Itaendelea …..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa