Kassim ni tofauti na wasanii wengi wenye kelele mithili ya wauza mitumba.

Kassim ni tofauti na wasanii wengi wenye kelele mithili ya wauza mitumba.

Uwanja umejaa kelele si wasanii si mashabiki katika uwingi kelele ni nyingi. Na kelele ni kero kwa wajuzi wa muziki, lakini kelele ni pendwa kwa kizazi cha Instagram. (Soni)

Na waswahili hunena yakuwa “Daima mwenye kelele hana neno” (Naam). Na ndiyo maana wasanii wengi hawana sifa za kusifiwa mbele ya muziki bali kelele za hovyo.

Na shangazo kuu ni kuonekana kupendwa na wengi, ilihali wajuzi hawajui wanaimba nini na inakuaje wanakuwa ni pendwa eti? (wasanii wenye kelele)

Lakini simamio la Kassim Mganga ni utulivu katika kelele za kufanya muziki, twanena tena yakuwa ni kelele za muziki. Na mswahili hunena yakuwa “Kuelewa ni kipaji pia) (Tafakari).

Kumetoka nyimbo nyingi mno katika nyakati hizi, na hakika huu wimbo ni bora toka kwa Kassim Mganga.

Na ubora wake ni katika mbinu za utulivu katika mikao ifaayo katika uimbaji kamili. Lakini utoaji wa sauti wenye ladha nzuri na lafudhi ya kipwani katika usikivu ni kitu pili.

Ila namna ya utamkaji wa maneno katika usahihi unaleta nogesho la ongezeko katika ukamilisho wa wimbo katika utatu.

Na upana wa kuzingatia ujumbe na sisitizo la uimbaji na muambatano wa ala za muziki hakika unaleta kolezo la uchanganyo wa uzao bora wa muziki katika unne!

Na sisi ni nani kiasi tusisifu wimbo huu wa ‘Silipizi’? Lakini kwanini tusisifu mapigo ya wimbo toka kwa Aloynem?. Hakika twasifu.

Ila ukamilisho wa video toka wa muongozaji Ivan unakamilisha nogesho la tazamo katika upana wa macho yetu.

#TuzungumzeMuziki