Kama wamlidanganya Rais kuwa studio ni tatizo, kipi kinashangaza kusema hiphop haiuzi?

Kama wamlidanganya Rais kuwa studio ni tatizo, kipi kinashangaza kusema hiphop haiuzi?

Kimsingi muziki huu ambao unaitwa Bongo fleva ambao sasa umeonekana kuwa biashara ni zao halali la muziki wa hiphop. Ila yapo mambo mengi ambayo yanachanganya juu ya neno bongo fleva na hiphop.

Miaka ya 1980-1990 hapa ndipo hiphop ya bongo ilianza kuchipua, na ilichipua kwa mtindo wa makundi.

Licha ya ufinyu wa media lakini kwa nguvu ya muziki wa hiphop hakika muziki huu ulisimama vyema na kuweza kubadili maisha ya wasanii wengi.

Wakongwe wengi wamekuwa wepesi kuiambia Tizneez Media kuwa “Muziki ulikuwa muziki maana hiphop imekomboa maisha ya wengi lakini pia imeweza kubadilsha maisha yetu kwa kiwango cha juu” ila hoja ya mdau kusema hiphop haiuzi sijui inatoka wapi.

Ni kweli usiopingika kuwa wakati muziki unaaza hakukuwa na mdau mwenye kujitwika madaraka ya kuamaua eti hii biashara wala hii si biashara. Tunaona sasa kadri siku zinavyozidi kwenda tunaona vile historia inavyopindishwa na huku mwanazuoni butu akichekelea maisha mafupi ya unafiki juu ya kufutwa kwa historia nzuri ya wakongwe walio wengi. Ama kweli “Mjinga muweke mbele ukimuweka nyuma utamsahau” ndio maana ya kusema “Jinamizi nyuma ya mwanazuoni”

Nguvu ya mdau imekuwa kubwa mno maana kila kukicha kundi la wasanii wa bongo fleva limekuwa likiamini zaidi katika mawazo ya mdau mmoja tu kuwa hiphop haiuzi. Ni mwaka jana tizneez tuliandika “Hakuna muziki usiokuwa biashara” kiuhalisia jambo hili lipo wazi.

Tunaona ni jinsi gani nguvu ya mdau ilivyopana, maana sasa hata vijana wake nao wamekuwa watoa mahubiri mema kuwa hiphop haiuzi. Hivi kweli hiphop haiuzi? Haiuzi kwa maana ipi? Album, matumbuizo au nini? Je wameipa nafasi? Maana biashara ni matangazo.

Ukitazama kwa undani hakuna sababu ya kuwaamini wala kumuamini mtu huyu ambaye amekuwa/wamekuwa wakijiweka mbele ilihali kinywa chake kimejaa maneno ya uongo.

Nguvu ya kuaminisha mashabiki kuwa hiphop haiuzi ni kubwa mno,  sijui ni kwanini uongo huu unahubiriwa kila leo.

Mashabiki wengi wamekuwa wakiamini uongo huo ambao hauna maana mbele ya watu makini. Lakini mashabiki inapaswa wajue kuwa watu hawa ambao wimbo wao ni kuwa hiphop haiuzi ndio hawa hawa ambao walimdanganya Rais kuwa kuna tatizo la studio.

Hivi kweli mwaka 2005-2010 kulikuwa na tatizo la studio? kuna vitu huwa vinaleta fedheha mno.

Itaendelea……..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Attachment