Kama wamlidanganya Rais kuwa studio ni tatizo, kipi kinashangaza kusema hiphop haiuzi? Sehemu ya II

Soma hapa sehemu ya I

Kama wamlidanganya Rais kuwa studio ni tatizo, kipi kinashangaza kusema hiphop haiuzi?

Soma hapa chini sehemu ya II

Kama wamlidanganya Rais kuwa studio ni tatizo, kipi kinashangaza kusema hiphop haiuzi? Sehemu ya II

Maoni yamekuwa mengi kwenye maandiko haya sehemu ya  I. Kama Team tizneez tunashukuru kwa maoni na hatupingi mtazamo wa mtu kama wengi wanavyofaya.

Lakini mashabiki hawajui yaliyomengi ambayo yanaendelea kwenye muziki, zaidi ya kuaminishwa uongo juu ya mambo mengi yanayohusu maisha ya kimuziki ya wasanii wengi.

Jambo baya zaidi ni uongo ambao umekuwa ukigeuzwa kuwa ukweli  tena mzuri, lakini uongo huo umekuwa ukiwanufaisha wasanii wachache tena kwa kiasi kidogo. Lakini bado wameukumbatia uongo huo.

Sawa tufanye kweli tulikuwa na tatizo la studio huo mwaka 2005 -2010 je studio iko wapi? Je!wasanii gani wanarekodi? Au kuna vigezo gani vimewekwa ili mtu aweze kurekodi? Je studio inasimamiwa na nani? Chama cha wasanii au mtu binafsi?

Jambo hili ni jambo zito na linahitaji ufafanuzi, ila wasanii wote wapo kimya.Nguvu ya wasanii wachanga kusifiwa na kupewa hotuba wasome bila kujali maslahi yao pia ni kubwa.

Tazama nguvu ya uongo ilivyo na maana mbele ya watu, lakini hapa ndipo inapopaswa ujue kuwa lengo la kelele za hiphop haiuzi ni kutaka pia uongo wao uaminike kwa jamii.

Siachi kusema Duniani kote hakuna muziki usiokuwa biashara, hivyo ukisema hiphop sio biashara hakika inabidi tukushangae kwa maswali mengi.

Wapiga kelele maarufu wa hiphop sio biashara ndiyo hao hao ambao kwenye matumbuizo yao wanawaleta wasanii wakubwa wa hiphop na kuwalipa pesa nyingi mno, sasa unasemaje hiphop sio biashara?

Hatupaswi hata kidogo kuamini kinywa chake mdau huyu, pia kama hiphop haiuzi kwanini hasemi kipi kifanyike ili iwe biashara? kwanini anasimamia hoja ya haiuzi tu?

Leo hii tuna watu wengi wenye uwezo wa kusaidia jinsi gani tunaweza kufanya hiphop ikawa kama aina nyingine ya muziki kwenye upande wa biashara. Kama lengo letu ni moja kwanini tusiwe na mijadala ya kutazama na kutatua jambo na liende sawa? Kwanini hawapo wazi katika maswala haya? Yapasa mjue lengo lao sio moja, lengo lao ni kutaka kabisa kuupoteza muziki huu, na hii ni tangu mwaka 2002.

Kwa nguvu ya hiphop imeendelea kuwepo mpaka sasa…….

Itaendelea……..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa