Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno ndivyo Ruby anavyoendelea kuanguka kimuziki

Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno ndivyo Ruby anavyoendelea kuanguka kimuziki

Kipaji  cha muziki alichobarikiwa nacho msanii chipukizi Ruby hakika ni kipaji cha hali ya juu. Lakini kipaji ili kiweze kukupa faida kinahitaji misingi mizuri ya kila leo katika ya Sanaa na nje ya Sanaa husika.(Uvumilivu na Nidhamu)

Huwezi kuacha kutaja jina la Ruby mara tu unapotaka kutaja wasanii bora chipukizi katika upande wa kike kwenye muziki wa bongo fleva.

Katika uhalisia Ruby ni bora Zaidi kuliko ya wengi ambao tunawasikia na sifa wanazopewa sio sifa stahili, ila ni ushikaji, mapenzi lakini upendeleo wa hali ya juu.

Kuanguka kimuziki katika muda mfupi kwa Ruby imekuwa ni jambo jepesi kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati na mavuno. Jambo hili halitufurahishi kama Team Tizneez kwa maana kipaji cha Ruby kinahitajika katika kuendeleza bongo fleva nzima katika Afrika lakini Duniani kote.

Bila umakini ataendelea kuishia kama upepo uvumao pembezoni mwa fukwe za bahari ya hindi.

Ila katika ukweli na uwazi kuna mambo matatu ambayo kwa upana yameweza kumuangusha Ruby kimuziki.

Kuwa msanii wa Efm, hii picha iliyoko kichwani kwa mashabiki wengi yakuwa Ruby ni msanii wa Efm. Jambo hili limefanya Ruby kukosa nafasi nzuri katika upande wa Media nyingine. Ila katika uhalisia Efm hawana msanii na Ruby hakuwa msanii wa Efm ila yeye alijionyesha kama ni msanii wa Efm.

Na hili likuja baada ya yeye kuwa tofauti na wapinzani wazuri wa Efm ambao ni Clouds Media Group, hivyo alijilaza katika ubavu wa Efm ila alipaswa kujilaza kwa media nyingine zote ili aweze kusikika vyema.

Fahari, ni wazi ufahari ambao amejivika ni kitanzi safi cha kunyonga kipaji chake mwenyewe. Ni mara Zaidi ya 3 Team Tizneez ilitamfuta shauri ya mahojiano ila fahari ya kujiona bora na kuchagua nani amuohaji nani asimuohoji.

Wakati huo akisahau kuwa sisi ndiyo watu wa kwanza ambao alitueleza yale yote aliyosema ametendewa na Clouds Media Group wakati wa msimu wa Fiesta 20/8/2016.

Lakini katika umri wake sidhani kama anafahamu msemo wa wehenga uliomwema yakuwa “Fahari mama wa ujinga”

Kuwa tofauti na Clouds Media Group hili ni jambo la tatu. Ni wazi ““Baniani mbaya kiatu chake dawa” licha ya mabaya yote aliyosema amefanyiwa na Clouds ila nguvu ya kusikika walikuwa wanampa ni kubwa mno. Haamanishi msanii hawezi kufanya vyema kama ataenda kinyume na Clouds hapana. La!Hasha uwe na uwezo wa kujiweza kufanya bila ya wao kwa maana ya kutokuwa tegemezi.

Katika upana wa mambo Ruby hakuwa amejiandaa katika kujitegemea bali kufanyiwa kila jambo wakati yupo chini ya uongozi wa  Tanzania House Talent.

Hivyo ni wazi kama ataamua kurekebisha mambo haya ni wazi tutaendelea kufaidi muziki wake kwa upana lakini akiendelea kufaidika vyema kipaji chake.

Ila yapasa ajue “Hasara humfika mwenye mabezo”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa