“Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili”

“Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili”

Kuna wakati yapasa tuseme ile kweli hata kwa lugha kali ilihali lengo ni kuweka usawa wa mtu kupata kutambua thamani yake. Lakini yapasa mjue enyi kizazi cha mitandao ya kijamii yakuwa “Vitabu vya Mungu ndiyo ufunuo, vya mzungu vitakuvua nguo”

Muziki umebadilika mara Muziki umekua hizi ni kauli pendwa kila leo kutoka kwa wale wenye mahala pakubwa pakusema. Neno mabadiliko ya muziki na muziki kukua wasanii wengi wamelipokea ndivyo sivyo.

Ingawa katika uhalisia muziki haujabadilika bali baadhi ya wasanii ndiyo wamebadilika. Imekua ufahari sasa kwa msanii kuonyesha maeneo fichwa ya mwili wake katika uwazi mbele ya jamii tena bila haya wala uoga.

Je!haya ndo mabadiliko ya muziki? au ni msanii husika ndiye amebadilika? au huku ndiyo kukua kimuziki? au ndiyo kwenda kimataifa?

Lakini waungwana yapasa mjue “Shati bovu si mgongo wazi” (Akili) Na daima “Usipoumiza akili utaumiza mwili”

Wasanii wengi wameegemea katika kufanya jambo baya ili tu wapate kuzungumziwa katika vyombo vya habari. Hivyo ni wazi akili ya ubunifu imepotea bali miili yao kubaki kuwa kama ndiyo mtaji wa yeye kufika mahala fulani.

Hiki ambacho kinaendelea kwa Malaika ndiyo ambacho amekitaka kuzungumziwa kuanzia ngazi ya mitandao mpaka kwenye Radio,Runinga na hata magazeti. Na kwake ni ufahari kuonyesha mwili wake, huku akisahau yakuwa “Fahari mama wa ujinga” Ila yapasa ifike mahala Media ziamue kuzima habari kama hizi mbele ya jamii, ni wazi ni ngumu kuzuia katika ngazi ya mtandao ila watu wa media kufunga vinywa vyao katika kujadili mada za wapiga picha za utupu.

Na kufungua vinywa vyao katika kazi nzuri ya sanaa ila kuwapa nafasi wale wenye nyimbo nzuri kusikika. Kwa maana mambo haya ya picha mbaya hayakuzi wala kusaidia lolote kwenye muziki wa kizazi kipya.

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment