‘Joseph’ wimbo wa Prof Jay wenye historia tofauti kwenye muziki wa kizazi kipya.

‘Joseph’ wimbo wa Prof Jay wenye historia tofauti kwenye muziki wa kizazi kipya.

#TuzungumzeMuziki na si jambo jingine, yapo mengi ambayo Prof Jay ameweza kufanya katika muziki huu wa kizazi kipya.

Kwa sasa Prof Jay ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chadema. Licha ya kuwa Mbunge lakini hajatupa kijiti cha muziki kwa maana ameweza  kutoa ngoma mbili tangu kuwa Mbunge. Nyimbo hizo ni kazi kazi na Kibabe, na zote zimeweza kufanya vyema.

Licha ya kuwa ni mmoja ya wasanii ambao wanaongoza kuwa na nyimbo nyingi zilizotamba kwenye ramani ya muziki lakini Prof Jay anabaki kuwa msanii pekee ambaye ameweza kutunga wimbo kupitia jina lake.

Jina lake halisi ni Joseph Haule, na Pro jay ameweza kutungia wimbo jina lake la Joseph ambapo haukuwa tu wimbo bali hata kubeba jina la album nzima.

J.O.S.E.P.H ni wimbo ambao ulifanyika chini ya mikono ya Majani ndani Bongo Record. Ambapo kwenye chorus alisimama Rama Dee.

Ni wazi Prof Jay ni msanii pekee aliyeweza kutumia jina lake na kuweza kuigusa jamii kwa namna ya tungo zake.

Ni wazi aina ya tungo hizi ni tungo ambazo hazipo sasa na kwa maono ni wazi ni ngumu kuzipata maana wasanii wengi wanapotoshwa na neno biashara.

Wimbo huu wa J.O.S.E.P.H ambapo kila herufu ilisimama na maana yake. J, Jifunze, O,ona, S, Sema, E, Elimika, P,Pitia, H, hamasika.

Lakini J.O.S.E.P.H ni album ambayo ilikuwa na nyimbo takribani 11, na nyimbo hizo ni, .Nikusaidiaje ft Feruz, Nimeamini ft Jaydee, Inatosha ft Mr Sugu, Vuta Raha, Border Kwa Border ft Naziz, Heka Heka Za Star, J.O.S.E.P.H. ft Rama Dee, Nisamehe ft Banana Zoro, Wapi Nimekosea ft Mandojo na Domokaya, Una ft Ngwea na Black Rhyno, na Hakuna Noma ft Inspector Harun na Simple X

Na album hii ni album ya tatu ya Prof Jay ambayo ilitoka mwaka 2006.

#TuzungumzeMuziki.

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa