Je! Wajua wimbo wa Zimbabwe wa Roma kiitikio kimeimbwa na wasanii 4 tofauti?

Je! Wajua wimbo wa Zimbabwe wa Roma kiitikio kimeimbwa na wasanii 4 tofauti?

Wimbo huu mpaka sasa unatimiza miezi 9 na siku 30 tangu kutoka kwake, huku ukiwa na watazamaji 1,957,930 katika mtandao wa ‘youtube’

Ambapo chanzo kikuu cha wimbo huu ni tukio zima la utekwaji wa msanii Roma Mkatoliki, ambapo alikuwa na wenzake akina Imma, Moni na Bin Laden.

Na walipatikana katika siku chache za mbeleni wakiwa na majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao, husasani zaidi Roma Mkatoliki.

Na mnamo 10.8.2017 msanii Roma Mkatoliki aliachia rasmi wimbo huu katika mtandao wa Youtube lakini kwenye vituo vya Radio na Runinga.

Na mdundo wa wimbo huu mtayarishaji ni Bin Laden chini ya studio za Tongwe Record.

Hakika wimbo huu ni wimbo ambao uliweza kupata usikivu mkubwa katika masikio ya wengi katika muda mchache tangu kutoka kwake.

Lakini Je! wajua yakuwa wimbo huu kiitikio chake kimeimbwa na wasanii wanne tofauti?

Ni wazi wengi hudhani wameimba watu wawili kama si mmoja, lakini katika uhalisi kiitikio cha wimbo wa Zimbabwe kimeimbwa na wasanii wanne, ambapo ni Magic (THT), Mellisa (THT),
Atan Voice, na Witty.

#TuzungumzeMuziki