Je! Nikki wa Pili wajua hekima ni kupaza sauti katika njia kuu?

Je! Nikki wa Pili wajua hekima ni kupaza sauti katika njia kuu?

Daima waswahili husema “Mwizi huenda na mwizi wakati mlevi na walevi” Kadhalika msanii Nikki wa Pili ambavyo amekuwa akienda sawa na wapenda hoja zenye maana na kujenga.

Ni wazi Nikki amekuwa ni mwenye kuandika mengi mitandaoni hasa kwenye kurasa zake.

Na wengi wamekuwa wakiyapokea maoni yake katika upana ulio mkubwa mno, hatuna hakika yakuwa yeye mwenyewe anajua namna ambayo maandiko yake yamekuwa na nguvu katika watu wengi.

Lakini kwanini hayafanyi haya katika njia yake kuu? Maana yapasa ajue yakuwa hekima ni kupaza sauti katika njia kuu.

Ni wazi kama Nikki wa Pili atapaza sauti yake katika njia kuu katika maandiko yake ya kwenye mtandao ni wazi heshima na mafanikio yake yatakuwa makubwa katika njia yake kuu lakini hata katika upande mwingine.

Na ni vyema ajue yakuwa macho ya watu wenye ufahamu mkubwa hutazama kile ambacho huandika hivyo kuna sababu ya hamisho la maandiko yale katika tungo zake ili awe na uwanja mkubwa Zaidi wa kueleza mengi kupitia muziki wake.

Lakini mara zote wimbo/nyimbo husambaa haraka na kueleweka haraka kuliko maandiko.

Hata nyakati ngumu na zakuhitaji ushawishi Fulani ni wazi nyimbo ndiyo hutumika nyema ili kufikisha ujumbe kwa wepesi na haraka Zaidi.

Hivyo ni vyema na ni wakati sahihi wa Nikki wa pili kuhamisha maandiko yake kutoka kwenye mtandao na kuleta katika njia yake kuu ya muziki.

Na yafaa ajue yakuwa “Mwacha asili ni mtumwa”

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa