Je! ni sawa kwa Nandy kuwapeleka wazazi wake kwenye Media?

Je! ni sawa kwa Nandy kuwapeleka wazazi wake kwenye Media?

Ni swali ambalo tumeulizwa mno na mashabiki nasi hatuna budi kuweka wazi katika ujibu wa wengi. (Ndiyo)

Mosi watu wanapaswa kujua kuheshimu maamuzi ya mtu ni jambo jema. Tunaamini Nandy ana uongozi imara kiasi cha kuamua wazazi waende kwenye Media kama sehemu ya utambulisho wa wimbo. (Eeh)

Na ni vyema mjue mashabiki swala hili ni mkakati katika mpango kazi wa utambulisho wa bidhaa (Wimbo) wa sasa kwa namna ya tofauti. (Mpango)

Lakini nini ambacho kimetokea? Hakika haiwezekani watu wakahoji kuhusu wimbo tu, lazima wahoji na maisha mengine nje ya wimbo huo. (Uhalisi)

Na sasa wapo katika mitandao kwa maana ya kuzungumzwa kwa upana. Na vipaza vimeshaanza kuwa vingi mbele ya vinywa vyao wazazi hawa. (Kabisa)

Lakini Je! wataweza kukabiliaba na vipaza hivyo ambavyo vingi havina maadili ya nini wahoji na nini wasihoji? (Ulizo)

Lakini kuwaweka wazazi katika mwanga wa Media maana yake ni kuweka maisha yao katika uwazi mpana. Je! wazazi nao wataweza kuishi maisha ya kusongwa na vipaza? (Ulizo tena)

Tunaamini Nandy anajua kero na namna ya kukabiliana katika hoji nyingi zaidi, Je! wazazi nao wanajua? (Ulizo)

Vivyo kuwaweka katika uso wa Dunia ni kuweka tabu katika upana wa uisho wa wazazi, lakini tunakumbusha kumbukumbu tu yakuwa “Tuheshimu maamuzi ya mtu” (Naam)

Tunaamini mno ataweka misingi ya wazazi wake katika uchaguzi wa kipi wazugumze na nani awahoji, tunaamini itakuwa hivyo. (Busara)

Kwaiyo kibiashara ni wazi ni sawa tu kuwapeleka kwa maana imeleta msukumo

wa watu kufutailia zaidi wimbo huo. 

Lakini kutaka kujua mengine mengi katika historia ya uleleo wa Nandy. Lakini daima “Muziki utaishi matendo yatapita” (Tafakari)

#MuzikiNiSisi