Je! ni sahihi kwa Darassa kusitisha matumizi ya mtandao wa Instagram

Je! ni sahihi kwa Darassa kusitisha matumizi ya mtandao wa Instagram?

‘Muziki’ 2016 ni wimbo wake ambao umefanya kila mwenye sikio asikie wimbo huo na kujua upana wa Darassa katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Lakini ‘Sikati tamaa’ ni wimbo wake ambao ulimtambulisha vyema kwa wajuzi wenye kujua upana wa muziki.

Licha ya wengi kumfahamu zaidi 2016 lakini Darassa yu imara tangu 2010.

Na 12.8.2017 Darassa aliacha rasmi kutumia
mtandao wa picha (Instagram). Na mpaka sasa ni takribani mwaka mmoja na mwezi tangu alipoacha kutumia.

Na ni wazi katika nyakati hizo ameweza kuwa na mpishano mpana wa fedha katika hali ya matangazo ya makampuni mengi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hususani Instagram.

Na leo tumeona vile alivyofanya maamuzi kabisa ya kusitisha matumizi ya mtandao wa Instagram.

Jambo hili si sahihi katika kazi yake ya muziki maana mtandao ni katika njia mosi ya matangazo mengi ya muziki wake.

Lakini kitendo hiki cha kusitisha matumizi yake kinazidi kumpotezea mashabiki wake. Maana hata katika posti yake ya mwisho mashabiki wake waliendelea kuandika mengi katika kuonyesha hisia zao juu yake.

Ni nani mshauri wa Darassa? au Darassa ndiye mwenye kushauri washauri?. (Soni)

Kitu ambacho Darassa anapaswa kujua ni kwamba ukimya hauwezi kuwa mkombozi wake katika yote ambayo yapo juu yake.

Na mswahili hunena yakuwa “Mkia
haungozi kichwa”. Lakini daima “Si busara kukimbia mvua kwa kujitumbukiza mtoni”

La! hasha Ila mswahili anasisitiza yakuwa “Tusisukume gari lisilo na magurudumu” Tafakarii..

#TuzungumzeMuziki