JE! LINEX HAAMINI KATIKA MUZIKI WAKE?

rsz_linex

JE! LINEX HAAMINI KATIKA MUZIKI WAKE?

Linex ni msanii mwenye kipawa kikubwa, tizneez ni moja ya kati ya watu wanaoamini kuwa kipaji chake bado hakijamlipa kama vile ipasavyo, maana amekuwa akiandika nyimbo zenye kuishi kwa muda wote tofauti na wasanii walio wengi wakitoa nyimbo zao huwa hazimalizi hata mwaka mmoja zinakuwa tayari zimepoteza radha kabisa.

Linex yuko tofauti na wasanii walio wengi hapa nchini, kuanzia style yake ya uimbaji na hata utunzi wake. Amekuwa akiteka hisia za walio wengi pale anapoingizia maneno ya Kiha katika tungo zake.

Kwa hela ni wimbo wake unaofanya vizuri sasa katika kila media hapa nchini. Kama ilivyo kawaida yake Linex hakuacha kutupa radha ya Kiha katika wimbo huu “Uhuru mwana yaya gende muwage” ni wazi amenogesha zaidi wimbo huu kwa kibwagizo hiki, na hii ni maana halisi ya sanaa.

Sitaki kuamini wala kufikiria kama Linex hajui ukubwa wa nyimbo zake au haamini katika muziki wake, hili linanipa mashaka kwa matendo ambayo siku hizi aimeonekana kuyafanya mara kwa mara. Iliwashangaza zaidi walio wengi siku ambayo alikuwa kwenye mahojiano katika kipindi cha usiku cha runinga, ambapo alimshambulia Adam Juma ambaye ni moja kati ya waongozaji wa video hapa nchini. Mashumbilo hayo yalikuja kwa kile alichodai Linex kuwa muongozaji huo ameharibu video yake. Lakini haikuishia hapo bali iliendelea mpaka kwenye mitandao ya kijamii.

Siku chache mbele Linex alifanya tena yale yale aliyofanya mwanzo kwa Adam Juma katika kituo cha runinga tena katika kipindi cha usiku. Na vita hiyo ikaendelea tena katika mitandao ya kijamii kama ilivyo desturi ya walio wengi hupenda majibizano yasiyo na tija kwenye mitandao ya kijamii hususani mtandao wa picha (Instagram) basi walipata wasaa mzuri wa kujibizana na muongozaji wa video Adam Juma. Lakini haikuwa kama wengi walivyozoea isipokuwa Adam Juma alitumia hekima ya kuomba radhi kwa Linex na kumtaka amsamehe na hata kusema hatokuja kuendelea na majibizano hayo tena katika maisha yake.

“kutafuta kick” maneno hayo yamekuwa yakimaliza wasanii wetu kisanaa. Maana wamekuwa wakifanya mambo mengi ambayo yatafanya yazungumziwe zaidi katika mitandao ya kijamii hata kwenye baadhi ya media ambazo mara nyingi zimekuwa zikipenda na kushadadia mambo yasiyo na msingi. Lakini hasara za kutafuta kick ni kubwa tofauti na ile kick utakayoipata. Leo tumeona kuna wasanii wanakuwa mabalozi katika makampuni mbalimbali nadhani hakuna kampuni inayotaka msanii asiye na nidhamu ndani ya kazi yake na hata nje pia.

Wengi hupenda kick ya mitandao zaidii, Ingawa siamini katika kuzungumziwa mitadaoni au media lazima ufanye jambo ambalo ni kinyume na kile ukifanyacho. Hata mambo mazuri pia hupewa nafasi na pia utajijiengea heshima kila iitwapo leo.

Mapema jana kupitia mtandao wa kijamii Twitter msanii Linex aliandika”Barnaba nimekuwa nikikuamini kwenye utunzi na uimbaji lakini why unakimbia kukutana na mimi kwenye wimbo mmoja na mdau kaweka dau.”

Hivi kweli kulikuwa na haja ya kuandika hayo katika mtandao wa kijamii? Je hakuweza kumtafuta Barnaba wakajadili wakiwa wenyewe bila mashabiki kujua? Au ametaka kuonekana bora zaidi kuliko Barnaba?. Team tizneez ilihoji tangu jana!!siku wanayokutana na mdau pamoja na Barnaba waliandika katika mitandao ya kijamii?

Ni wazi baada ya maandiko ya linex ikawa gumzo katika mitandao ya kijamii haswa Instagram, hivi ilikuwa na umuhimu wa kuandika hayo kwenye mitandao?

Napata mashaka na Linex kwa kile kinachoonekana sasa anavunja heshima yake aliyoitengeneza kwa muda mrefu, ikumbukwe Linex hakuwa msanii wa kuropoka hovyo katika media wala kwenye mitandao ya kijamii. Sasa wakati huu amekumbwa na nini? Mbona anapotoka kila leo? Je haamini katika muziki wake? Hivyo anafanya mambo ambayo yanaweza kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii, wengi husema kick! Je ni kweli anatafuta kick? Je kufanya hivyo inamsaidia? Kuna maswali mengi ambayo majibu yake hatuna maana siri iko rohoni kwake.

Kuna haja ya kutumia mitandao ya kijamii kutangaza kazi yako zaidi kuliko kuanzisha malumbano yaisyo na tija ambayo kiukweli yatashusha thamani ya muziki wako. Muziki wako ni bidhaa kubwa ambayo kila umri umekuwa na mashabiki.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez