Je! Kuna usahihi wa Diamond Platnumz kuchorwa kikaragosi?

Je! Kuna usahihi wa Diamond Platnumz kuchorwa kikaragosi?

Mosi Sanaa ya uchoraji ni ya kuweka alama kwa kutumia vifaa mbalimbali vya kuchorea ambapo penseli ni moja wapo, lakini kalamu ya wino, brashi, makaa, na vitu vingine vingi hutumika kukamilisha mchoro/picha.

Ingawaje katika nyakati hizi michoro pia huchorwa kwa kutumia kompyuta katika kutumia viwezeshi vingi vya kuwezesha uchoraji huo kwa kumpyuta.

Ambapo wajuzi wanaamini yakuwa uchoraji wa kutumia kompyuta ni njia rahisi zaidi ya uchoraji. (Usasa)

Na daima tokeo la uchoraji huitwa ‘Mchoro’ au ‘Picha’. Lakini zao la picha/mchoro ni katika tafakari ya mchoraji juu ya ujumbe ambao ametaka kufikisha.

La! Hasha uchoraji ni Sanaa kama zilivyo Sanaa nyingine katika upana wa uwasilishi wa ujumbe kwa hadhira. Ila mwenye kufanya Sanaa ya uchoraji daima huitwa mchoraji.

Maswali ni mengi kwetu katika mchoro/picha ya kikaragosi chenye mfanano na msanii Diamond Platnumz, ambapo wengi wameuliza je!ni sahihi Diamond kuchorwa kikaragosi?.

Sasa katika swala zima la uchoraji kuna aina nyingi za upana wa mchoraji katika fikisho la ujumbe wake kwa hadhira juu ya picha/mchoro chorwa.

Na hapa huzaa tegemeo la mchoraji katika upenzi wa aina ya picha/mchoro wenye kumvutia yeye. Nyakati nyingi Sanaa ya uchoraji haitazami mno upana wa ujumbe bali kumvutia mtazamaji katika chekesho tu au raha ya macho katika tazamo la nyakati zote.

Na mara nyingi picha za vikaragosi ndizo huleta chekesho kwa wengi, hivyo kwa upana wa Sanaa ya uchoraji, mchoraji hulazimika kutumia jambo la nyakati zilizopo katika mchoro wa kikaragosi ili kuleta chekesho kwa watu.

Hivyo hakuna ubaya katika uchorwaji wa kikaragosi katika mfanano wa Diamond. Mchoraji amefanya Sanaa yake kama ambavyo wengine hufanya Sanaa zao kwa uwezo wao.

 

#TuzungumzeMuziki

Picha ya Kikaragosi ila hatujaweza kufahamu mchoraji wa picha hii