Je! Fid Q ni msanii mkubwa asiejielewa? Sehem ya II

Soma sehemu ya kwanza hapa

Je! Fid Q ni msanii mkubwa asiejielewa? Sehem ya I

Sehemu ya II soma chini

Je! Fid Q ni msanii mkubwa asiejielewa? Sehem ya II

Upana wa semi ya ‘kujielewa’ ni mkubwa kwa maana ya utambuzi wa kujua namna ya wewe/yeye ulivyo/alivyo katika uhalisi wa uisho wako/wake kwenye mengi. (Muziki)

Na kwa Fid Q tunaweka tazamo kwenye uendeshaji wa biashara yake ya muziki na ukubwa wake kwenye muziki. (Kujielewa).

Kiukweli hili limempita pembeni kaka yetu Fid Q na hapa ni katika tazamo la ‘Kitaa Olojia Album’ miaka mitatu ya ahadi na ahadi isitimie ikabaki ahadi tena. (Soni)

Lakini swali la msingi, hivi kweli msanii mwenye kuelewa upana wa album katika mauzo anaweza kuposti tangazo moja tu la album yake?. Ni wazi Fid Q ameposti mara moja na hiyo ni katika upana wa kuwaambia mashabiki wake juu ya awali ya album. (Chekesho).

Msanii mwenye kuweka tangazo mara moja ujue ni msanii ambaye ana ujazo wa mashabiki katika kila kona ya Dunia. Lakini msanii huyo hata acha kuipromote posti hiyo katika upana wa kufikia wengi zaidi. (Promoted post)

Kwanini Fid Q hakujifunza kupitia Wakazi? Simamio la matangazo ya Wakazi mpaka uzinduzi ilikuwa ni katika upana kamili wa biashara na hakika amefanikiwa. Na Fid alikuwepo katika uzinduzi wa album ya ‘Kisimani’ ya Wakazi, ina maana hakuna alichong’amua kupitia Wakazi?

Je!uzinduzi wa One The Incredble katika album yake fupi hakumfunza kitu Fid Q?. Hakika shangazo mbele ya wajuzi ni katika hali ya ukubwa.

Swali kuu Fid Q yeye anakwamisha na nini?. Ikiwa kijana mdogo Wakazi na One wameweza kufanya kwa ukubwa yeye anashindwa nini?. (Fedheha).

Sisi hatutaki kusadiki kabisa semi ya wajuzi yakuwa ni “Fid Q ni msanii mkubwa asiejielewa”.

Tarajio la wengi ilikuwa siku ya uzao wake wa 13.8.2018 kungekuwepo na album, lakini tulishawajuza watu yakuwa album itoke kimya kimya kwa maana ipi?. Maana kulikuwa hakuna dalili za kutoka bali tulijipanga kuidharau iabu juu yake kutoka kwa wajuzi wa muziki.

Nyimbo mbili alizotoa kwa mashabiki hazikuwa na uhitaji kushinda album kamili, lakini kwa ukubwa wake album ingetoka ilipaswa na inapaswa kufanya shoo nyingi zaidi katika Mikoa mingi zaidi awezavyo katika uuzo wa album lakini hata mwanzo wa tamasha lake.

Kwa nafasi ya Fid Q haipaswi iwe ni msanii mwenye kusubiri Fiesta, Komaa Concert na hata simu za mapromota wengi wa mikoani, bali shoo yake yenye ujazo wa faida kulingana na ukubwa wake.

Na simu za mapromota iwe ni ziada lakini si lazima kuzisubiri kwa nafasi yake ambayo yuko nayo kwenye muziki. Na daima yeye husema “Thamini huu muda kabla haujageuka histori’  sasa anakwama wapi kuishi katika semi yake?.

Lakini pia hunena yakuwa “Ni vyema kujifunza mengi sio kujua kila kitu” na mswahili nae asisitiza yakuwa “Ukijua upande huu upande huu haujui” basi yapasa awe na mtu nyuma yake mwenye upana wa biashara ya muziki na muendelezo wake.

Maana kujua muziki katika kuufanya ni jambo mosi, pili ni kuufanya huo muziki kuwa biashaara. Na hapo kuna mkwamo kwa wasanii wengi mno akiwemo Fid Q.

Fid Q mwenyewe atajingusha vyema katika ahadi za upekee asizoweza kuzitimiza na mwisho wa siku inabaki fedheha juu yake lakini wajuzi wa muziki wenye kumsifu vyema.

“Muda si rafiki wa mwanadamu atakukosha mavumba kama haupo on time” semi hii imetoka kwenye kinywa chake, lakini mbona anashindwa kuishi katika semi zake nyingi?.

Itaendelea….

#TuzungumzeMuziki