JAY MOE NA HILI GAME Sehemu ya III

Jay_Mchopnga

JAY MOE NA HILI GAME

Sehemu ya tatu
______________________

Kama bado hujaelewa katika mfululizo wa makala haya yamelenga nini?. Makala haya yamelenga kuuchambua wimbo wa Hili Game wa Jay Moe na wala hayajalenga kuelezea historia ya maisha ya Jay Moe kama baadhi ya watu wanavyodhani. Kila hoja iliyozungumziwa iwe inamhusu Jay Moe, Mtu mwingine au tukio lolote ina uhusiano wa moja kwa moja na wimbo wa hili game. Ni vema wakosoaji wausikilize wimbo kwanza ndio wachangie.

Hili game ya Jay moe ni tofauti sana na Hili game ya Juma Nature. Utofauti wake ni kwamba Hili Game ya Juma Nature maudhui yake yamezungumzia changamoto za utafutaji wa maisha kwa ujumla wakati Hili Game ya Jay Moe imezungumzia changamoto utafutaji wa maisha kupitia muziki na maisha ya wanamuziki kwa ujumla.

Kwa hiyo sikushangaa pale Jay Moe aliposema kwamba hili game “sio tena tafu kama Nature alivyoimba”. Hapa nilivyomuelewa ni kwamba Game bado ni tafu ila utafu wake ni tofauti na nyakati za nyuma hususani wakati Nature anatoa wimbo wake.

Utofauti upo bwana! Wakati ule Dj Venture alimfuma marehemu YP akitembea kwa miguu kutoka Temeke mpaka Chuo Kikuu lakini siku hizi “msanii studio anakwenda na ndinga”. Kwa hiyo zamani wasanii sio tu walikuwa hawana magari bali hata nauli za daladala ilikuwa tabu. Leo kuna baadhi ya wasanii hawapigi show bila kuwapa Milioni tatu. Kwenye hiyo millioni tatu, Laki Tano itaishia kwenye mafuta na service so asipopata show gari litashinda “parking” kuliko barabarani.

Ila nilishangaa kidogo niliposikia kibwagizo kikichagiza kwamba Jay Moe amepita kwenye msoto. Kibwagizo hiki kikanifanya nikumbuke miaka kadhaa iliyopita nilipata kumsikia Jay Moe katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha Redio akisema kwamba yeye hakuwahi kusota kihivyo kwenye harakati za kutoka, ilikuwa rahisi kwa yeye kukubalika. Mshangao wangu ukaondolewa baada ya kuikumbuka ile dhana kwamba “msoto ni msoto tu haijulishi mkubwa au mdogo”.

Nikashangazwa tena na Jay Moe aliposema kwamba “Game haiendi bila AJ na Nisha”. Nikawaza huyu Jay Moe hii game anaijua vizuri kabla hajaanza kuicheza ni vipi leo Game haiendi bila AJ na Nisha ina maana katika wote amewaona hao wawili tu ambao kiuhalisia sio watu ambao wanaweza kufanya game ya mtu fulani isiende kama Jay Moe alitaka kumaanisha wakwamishaji.

Pengine kwa mtazamo mwingine labda Jay moe alitaka kumaanisha video yako haiwezi kupata promo kama haijafanywa na AJ au Nisher. Huu ni wakati ambao wasanii wanafanyia video zenye ubora mzuri kuliko audio za nyimbo zao. Jay moe sijui kama ndio alikuwa anakazia ule mstari wake kwamba “wasanii hawasifiwi kwa mistari tena nowadays kichupa”

Huu ni wakati pia ambao tunaambiwa kwamba bila kuwekeza pesa game ya bongo haiwezi kukulipa. Najiuliza tu msanii ambaye hana pesa ila ana kipaji anaweza kutoka vipi, maana studio maprodyuza wanataka pesa na ngoma ile ipate “Air Time” mpaka iwe “Hit Song” inahitaji msanii afungue wallet kisawasawa kwa madj/kituo cha redio ili wimbo uwekwe kwenye rotation (mzunguko). Kama una wimbo mzuri alafu huna pesa hapo subiri kudra za Mwenyezi au fadhila za meneja. Mwisho wa siku naweza kukubaliana na Jay Moe anaposema kwamba wasanii ” Wachache ndio wenye vipaji, Nao ili watoke wanahitaji mtaji”

Kwa wenzetu hali kama imetatuliwa na mfumo wa kuwa na “Record Label” ambapo msanii akiwa chini ya Lebo majukumu yote hayo na mengineyo yanatekelezwa na Lebo husika aliyopo kulingana na makubaliano. Mfumo huu kwa Tanzania umefeli kutokana na mfumo mzima wa soko la muziki kum-favour msanii kuliko watayarishaji/studio. Wenye studio ndio wanaohangaika kukuza wasanii lakini mwisho wa siku hawanufaiki na chochote. Baada ya mkataba na msanii kuwa juu huwakimbia maprodyuza na wasanii kuendelea kutumia kazi zile zile bila kuwalipa maprodyuza. Kwa mfano tu Ukipata muda muulize Mona Gangstar alichofaidika/anachofaidika kwa kum-manage Young Killer.

Hii dhana ya kuamini kwamba pesa ni kila kitu Muda mwingine inaweza kumfanya mwenye kipaji cha kawaida kuonekana ana kipaji kikubwa, mwenye kipaji kikubwa asisikike na asiye na kipaji kusikika. Dhana hii imetumiwa vibaya na Said Fella pale Jay Moe anaposema siku hizi Said Fella sio meneja tu bali ana kipaji. Sio huyo tu kuna yule meneja wa watanashati aliyefanya wimbo na Young Killer. Walichofanya mameneja hawa kwa sababu tu wana uwezo wa kupeleka ngoma redioni zikachezwa hawana tofauti na wale washkaji zake Fid Q ambao huwa wanafanya nyimbo mbovu mpaka wao zinawapa uvivu kuzisikiliza.

Itaendelea……

www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez

 

Imeandikwa na

Malle Hanzi
0715076444
©2016.