Jambo kuu linalowangusha wasanii wengi wa hiphop ni mfumo wa uendeshwaji muziki na madereva wakuu.

Jambo kuu linalowangusha wasanii wengi wa hiphop ni mfumo wa uendeshwaji muziki na madereva wakuu.

Hakuna ubishi yakuwa Tizneez Media Group ni sehemu kuu ya kuzungumza muziki wa hiphop kwa upana zaidi.

Na nyakati zote tumekuwa tukisamama katika kweli bila kujali kile wasemacho yakuwa “Hiphop haiwezi kuwafanya mkapata mafanikio” hayo ni maneno ya wachambuzi wengi ambao wamekuwa wakitafuta nafasi kwa madereva wakuu wa muziki.(Fedheha).

Hivyo kukosoa jambo ambalo halipo sawa juu ya madereva hawa kwao ni ngumu kwa maana ya hofu ya kukosa mengi yenye mema kutoka kwa madereva.

Lakini yapasa ujue “Utu busara, ujinga hasara” Lakini tunawakumbusha tena “Hofu haina msaada zaidi ya kukuvuruga akili” lakini ndugu zetu yapasa mjue “Maisha ya uongo hayawezi kuwa marefu”.

Mfumo wa madereva wakuu wa kwenye muziki ni mfumo ambao unataka msanii asiwe na sauti mbele yao.

Watakalo wao ndiyo ufanye kwa wakati wao, hata kama hoja yao ni dhaifu ukiwapa hoja yako watasema “Anajifanya anajua sana” (mjuaji)

Wasanii wengi wa hiphop wafuata misingi sio wasanii wa kutaka kufuata madereva wanataka nini, hivyo misimamo yao inafanya kunyimwa kabisa nafasi. Mfumo ulivyo ni kwamba ukikubali wakufanye watakavyo kwa hakika utakuwa kinara katika muziki huu. Na tunaona namna ya wasanii ambao uwezo wao ni mdogo walivyoweza pewa vyeo kwenye muziki

Lakini kama tu utakuwa huendi sawa kwa kutambua haki zako zaidi kwa hakika utakuwa adui mzuri wa madereva hawa na kwa hakika wataziba mianya yote ambayo itaweza kumkomboa msanii.

Hivyo mfumo kandamizi ndiyo mfumo tawala ambao upo kwenye muziki wa kizazi kipya na wasanii wengi ambao unawasikia vyema ni wale ambao wamekubali msemo wa Kiswahili usemao “Mtumikie kafiri upate ujira wako”

Na wale ambao huwasikii ni wale ambao wamegoma kufuata uhalisia wa msemo huo. Na wala haipaswi kuwashangaa kwa maana kusimama katika ukiaminicho ni jambo lenye maana Zaidi katika maisha yote.

Lakini ni vyema wasanii hawa kujikomboa kwa nguvu ya mtandao kwa maana ya sasa muziki ukifanya kwa nguvu ya mtandao ni wazi utakupa mafanikio pia.

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa