Ipi ni sababu ya Mwasiti kupinga kauli za Linex juu ya utunzi wa wimbo wa Leka Dutigite 2012?

Ipi ni sababu ya Mwasiti kupinga kauli za Linex juu ya utunzi wa wimbo wa Leka Dutigite 2012?

“Tuanze na kuwatambua watunzi wa nyimbo ili tusogee zaidi kimuziki” Andiko hili tuliandika 9.4.2018. Na hii kabla ya Linex kuanza lalama juu ya kutaka kutambulika yakuwa yeye ni mtunzi halisi wa wimbo wa Leka Dutigite wa Kigoma All Star.

Ambapo wasanii kama Mwasiti, Diamond, Ommy Dimpoz, Baba Levo, na wengine wengi walishiriki kwa ukubwa.

Ambapo Mwasiti baada ya kusikia malalamiko hayo hakusita kuweka wazi yakuwa “Namshauri Linex aache kuongelea mambo yaliyopita” Na hayo aliyasema katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm. Ingawaje Mwasiti huenda akawa hajui yakuwa “Liandikwalo, halifutiki”. Lakini ipi ni sababu ya Mwasiti kupinga kauli za Linex juu ya utunzi huo?

Kwanini aache kusema yaliyopita? Kwanini asiseme katika kuweka usawa wa heshima za watunzi?

Na Linex amefanya endelezo la kujitangaza yakuwa yeye ndiye mtunzi wa wimbo huo, na hii ni katika kipindi cha The Base cha Itv jana.

Lakini lazima tujiulize kwanini Linex anataka zaidi hiyo sifa ya utunzi katika nyakati hizi? ikiwa kazi hiyo ifanyika 2012, na kuweka katika mtandao wa Youtube mnamo 31.7.2012.

Ilihali yapasa tuanzie katika chimbuko la kujua yakuwa nini maana ya mtunzi, na hii ni katika kuleta usawa.

Mtunzi wa nyimbo ni mtu aliyebuni chanzo cha wimbo na muendelezo wake. Na humpa msanii/wasanii aweze/waweze kuingiza sauti kupitia tungo hizo kwenye studio za kurekodi sauti.

Na nyakati zote mtunzi hupewa sifa kwa uwezo wa kuwaza/kutunga uzao wa wimbo.

Lakini haki ya mtunzi husemwa hadharani katika kumpa heshima ya utunzi katika wazo kuu. Lakini katika nchi zilizoendelea kimuziki mtunzi hulipwa fedha juu ya zao lake la wimbo.

Ingawa wapo watunzi ambao wao hutaka kutambulika tu, lakini hao ni katika nchini yetu ya Tanzania tu.

Je!Linex anajinenea mwenyewe katika mtako wa jamii ya muziki wa kizazi kipya kumpa heshima?.

Maana katika kweli hatujawahi kusikia katika wasanii wote shiriki katika wimbo huo kunena juu wazo kuu ni la msanii Linex? Nini kipo juu ya swala hili? uhalisi uko wapi?.

Maana nguvu atumiayo Linex kusema yeye ni mtunzi wa wimbo ule ni zaidi ya kuzungumza wimbo wake mpya wa sasa. Kwanini imekuwa ni katika nyakati hizi? na si nyakati za wimbo ule kutoka?

Lakini kabla ya yote haya, makubaliano ya utunzi wa wimbo huo yalikuaje? Kwamba mtunzi atapewa sifa hiyo hadharani? au atapewa fedha? au itakuaje?.

Lakini je! swala hili linamnyanyua Linex kimuziki? ni wazi hapana maana ni jambo lilipita katika nyakati, hivyo hapo anabomoa vyema kundi la mashabiki ambalo walipata katika wimbo ule, ilihali hata umoja wa wasanii shiriki.

Jambo jema ni katika makubaliano ya mwanzo kama alifanya kwa mlengo wa kutaka tu wakamilishe kazi hiyo basi haina haja ya kuendeleza kuzungumza swala hilo.

Lakini kama yapo makubaliano yakuwa atajwe na wasanii husika basi kuna kila sababu ya kunena hadharani maana ni katika makubaliano. Lakini pia kuna nyakati yapasa Linex ajue yakuwa “Mvumbika changa hula mbovu” Tafakari.

#TuzungumzeMuziki