Inashangaza kumshangaa Baraka Da Prince

fYm97mIz_400x400

Inashangaza kumshangaa Baraka Da prince

Huwezi kutaja majina ya wasanii chipukizi wanaofanya vyema katika ramani ya muziki wa kizazi kipya bila kutaja jina la Baraka Da prince. Baraka amekuwa akifanya vizuri kimuziki ndani na nje ya Tanzania.

Ni siku kadhaa zimepita ambao kuna kipande cha video kilisambaa katika makundi ya WatsApps na hata katika mtandao wa picha “Instagram”.

Kipande hicho cha video kilikuwa kikimuonesha msanii Baraka Da Prince akiwa katika mahojiano kwenye kituo cha Mtv. Ambapo katika mahojiano aliongozana na mpenzi wake ambaye alikuwa ni mkalimani wake katika mahojiano hayo.

Maana ya kuwa na mkalimani wake ni kwamba hayupo vizuri katika kuzungumza lugha iliyokuwa inatumika katika mahojiano hayo ambayo ni kingereza.

Nianze na kumsifu Baraka siachi kusema yeye ni shujaa. Namsifu katika mambo matatu tu.

Jambo la kwanza kuwa mzalendo katika lugha yake ya taifa, pili kumtumia mpenzi wake katika kufanikisha jambo lenye kumtangaza kimuziki, na la tatu ni kuwa muwazi kwamba hayuko vizuri katika lugha hiyo ambayo ilipaswa kutumika zaidi kwenye mahojiano . Nimpongeze katika hayo, maana wengi wao hulazimisha na hatimaye huishia kuuma maneno na kukosa kufikisha kile alichopanga kukifikisha kwa mashabiki wake.

Katika siku 5 ambazo zimepita tangu kusambaa kwa video hiyo ambayo sikuona tija wala maana ya watu kumdhihaki Baraka eti hajui kingereza. Hii limenifanya niwashangae baadhi ya watu ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kumkejeli Baraka.

Video hazikupostiwa katika mtandao wa picha “Instagram” na mashabiki pekee bali hata watu wenye umaarufu waliposti. Ila katika posti hizo wapo ambao waliposti katika kusema sio jambo baya alilofanya. Na katika uhalisia sio jambo baya wala dhambi mtu kuto kufahamu lugha nyingine. Ila itakuwa jambo baya kama hufahamu wala hujui lugha ya taifa lako.

Inashangaza kuona baadhi ya watu maarufu wakiwa mstari wa mbele katika kumkejeri Baraka Da Prince. Idris Sultan ni moja kati ya wale wengi, ila sidhani kama anayo sababu ya msingi za kuweka kejeli juu ya Baraka.

Nimetazama posti yake Idris Sultan katika mtandao wa picha “Instagram” na nimejiuliza maswali mengi. Kipi kinachomchekesha juu ya Baraka kutokujua kingereza?, lakini pia juu ya ufahamu wake Idris, sitaki kusema kama ufahamu wake ni mdogo, bali ni vyema kutafakari kabla hujatoa kejeli kwa mtu na pia kuweka kitu katika mtandao wa kijamii ili upate comment nyingi na likes.

Leo tumeshau msanii Cabo Snoop alipokua Tanzania mwaka 2011-2012 ambao aliambatana na mkalimani wake maana hakuwa anajua kingereza wala Kiswahili bali kireno. Na aliweza kufanya mahojiano katika vituo vya radio na runinga vikubwa. Sasa leo hii kipi kinafanya tumkejeli Baraka?

Pia tusiahau hata wakati Fally Ipupa anachukua tuzo ya Mtv alizungumza Kifaransa maana ndio lugha ya taifa lao. Pia kwenye mahojiano yake huenda na mkalimani wake maana hajui kujieleza vyema katika lugha ya kingereza.

Ila nikirudi katika posti za watu maarufu mitandaoni inanifanya nikumbuke wimbo wa Nash Mc unaoitwa” “Naandika ambao ulitoka mwaka 2014. Ambapo kuna mstari alisema “Naandika kuhusu matumizi ya Kiswahili kwenye fani ya ushauri cha nini kingereza fikiri tumia akili fikra sahihi huja kwa lugha asili”

Kama fikra huja kwa lugha asili kwanii nisiwashangae wanaomshangaa Baraka Da Prince?

Ni ukweli usio kificho watu wengi maarufu wamekuwa ni watu wa kujikweza zaidi katika majukwaa mbalimbali katika kutumia lugha ya kingereza. Ni mara nyingi tumeona katika nchi za wenzetu watu wao maarufu hutumia lugha zao za taifa katika majukwaa mengi, ila kwa watu maarufu kutoka Tanzania naona imekuwa ni jambo gumu mno kutumia Kiswahili.

Si jambo baya kama unajua lugha hiyo ya kingereza ila ni jambo baya kumcheka mtanzania eti hajui kingereza. Huku ukisahau ni lugha ambayo inawezekana kujifunza.

Mtanzania amka thamini lugha yako, thamini kitu chako, kipe thamani ulichonacho.

Team tizneez inaamini katika kipaji cha Baraka Da Prince na tunategemea kumuona mbali zaidi ya hapa alipo tena katika kutumia Kiswahili.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez