Inahitaji uwe mnafiki mno kusifu wimbo wa ‘Muhogo’ wa Queen Darleen

Inahitaji uwe mnafiki mno kusifu wimbo wa ‘Muhogo’ wa Queen Darleen

“Wao watoto wa mjini daily mtawapenda na hamjui wanaimba nini” (Roho 7)

Alinena hayo miaka mingi iliyopita na semi hii ni yenye uhai mpaka sasa. (Muziki)

Lakini hawa hawa watoto wa mjini wanatujuza washamba cc @rhymesselassie yakuwa “Maisha bila unafiki hayaendi. (Shangazo)

Lakini kuishi katika uisho wa maisha ya unafiki ni kazi kubwa mno kwa sisi. (Hatuwezi)

Inahitaji uwe mnafiki hodari mno kusifu wimbo huu. Wimbo ambao ni wazi mdundo uko sawa lakini mchanaji/muimbaji ni chini ya kiwango haswa. (Soni)

Lakini wanafiki hodari wamesifu wimbo huu wa muhogo vyema tena sifa kubwa haswa. Ila ni katika “kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa” (Unafiki)

Kwa upana wa Wcb tunataraji @queendarleen_ kuwa bora kwa kupewa mitambao mizuri katika nyimbo zake. (Eeh)

Inatupa shangazo kubwa kuona anatoa wimbo ambao hauna ujazo kamili na amezugukwa na kundi la wajuzi wazuri wa muziki. (Ajabu)

Kwanini hawamwambii ukweli? wanataka wajuzi waendelee kuamini yakuwa uwezo wa Queen ni mdogo? (Hatujui)

Ni wazi nguvu ni kubwa katika matangazo ya wimbo huu, lakini nguvu hii inakosa nguvu kwa kuwa bidhaa haina nguvu mbele ya wengi katika ukamili wa wimbo. (Uhalisia)

Ni vyema Wcb wamshike Queen haswa katika ubebwaji imara si kumuacha katika endelezo la aina hii ya muhogo kana kwamba hawajali kuhusu toleo la bidhaa bora kutoka kwake. (Muda)

Na wenye kusifu wimbo huu wa muhogo hatushangazwi nao kwa maana hata mswahili hunena yakuwa “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” (Hakika)

#MuzikiNiSisi