“Ili muziki ukulipe ewe msanii”

“Ili muziki ukulipe ewe msanii”

Malalamiko juu ya wasanii ni mengi kuwa muziki haulipi, huku wachache wakionekana wakifaidika Zaidi na muziki huu wa kizazi kipya.

Tuzungumze Muziki ni kauli mbiu yetu na hapa tupo shauri ya Bongo Fleva na Hiphop, hivyo tuna kila sababu ya kuandika yote yanahusu muziki huu wa kizazi kipya.

Ni wazi malalamiko pekee hayawezi kutatua tatizo, bali tatizo hutatuliwa kwa kufanya maamuzi juu ya kuepuka au kuondoa kabisa tatizo hilo na si malalamiko ya aina yoyote.

Hakuna haja ya kulalamika kuwa muziki haulipi ilihali katika uhalisia muziki unalipa tena kwa kiwango cha juu. Ila wengi hukosea namna ya kufanya muziki huo uweze kuwalipa kama ambavyo unawalipa walio wachache.

Moja ya makosa makubwa wafanyayo wasanii wengi ni kufanya muziki kama kipaji na sio kufanya kama taaluma.

Huenda ikaleta mkang’anyiko juu ya kusema taalumu maana wengi hudhani taaluma ni lazima uende shule. Kiuhalisia si kweli kwa maana elimu “taaluma” inapatikana popote pale.

Hivyo ili msanii aweze kufaidika na muziki ni lazima afanye muziki kwa taaluma sio kipaji kama wengi wafanyavyo. Msanii hupaswi kuchukulia muziki kama kipaji pekee, inapaswa uchukulie kama taaluma ili uweze kutafuta wawekezaji.

Na msanii akifuta wazo la muwekezaji kumtafuta yeye msanii itamjenga vyema kimuziki na kimafanikio.

Msanii ni kiwanda cha uzalishaji wa muziki ni lazima ujue namna ya kumlinda mteja wako wako ambaye ni shabiki.

Pia kama msanii atamtafuta muwekezaji atafanikiwa tena na tena kwa namna ya mikataba ambayo ataingia nayo, ila kama muwekezaji akimtafuta msanii itakuwa ni kinyume kwa maana ya mikataba mibovu ambayo itamyumbisha msanii husika.(Mdau)

Mfano mzuri na hai ni nchi yetu ya Tanzania, ina kila aina ya madini lakini kosa ni kuchukulia kama tunu ambayo Mungu ametupatia. Hivyo tunasubiri wawekezaji watufuate na wakija wanafanya  kwa maslahi yao mpaka wanabeba vyote na tunaachiwa mashimo.

Hivyo hakuna haja ya msanii kusubiri muwekezaji wa kuwekeza katika muziki wako/wake, bali kutafuta muwekezaji mahala popote ili aweze kuendeleza maisha yake na maisha na muziki wake kiujumla.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

 

Attachment