Hivi miss Nigeria wanaweza kutumia nyimbo za Tanzania?

Hivi miss Nigeria wanaweza kutumia nyimbo za Tanzania?

Hakika ujuzi wa kujua ‘Jinsi’ na ‘Kuwa’ ni changamoto kwa wengi katika upana wa mengi yenye mengi hasa kwenye upana wa uhalisi wa uisho wa uzalendo.

Ni kheri ajuaye ‘Jinsi’ ya upana wa uzalendo lakini kheri nyingi kwa yule mwenye kujua ‘Kuwa’ ‘Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako”.

Na utumwa mbaya zaidi ni utumwa wa kutoa thamani kwa upana kwa kitu cha mwenzako ilihali wewe pia mjuzi wa kufanya hilo. (Soni).

Hakika ni fedheha kwa wote ambao wameweza kuupa uthamani muziki wa Nigeria katika jukwaa la Miss Tanzania. Kwa maana katika uwazi wa wajuzi ni kwamba Nigeria hawawezi na hawataweza kutumia nyimbo zetu kwenye Miss Nigeria.

Ni nani awezaye kunena Nigeria watakuja kutumia nyimbo zetu Tanzania katika jukwaa lihusulo Miss Nigeria? Na tumuone hapa akitupa uthibitisho.

Daima Nigeria wamejaa uzalendo wa hali ya juu na wanajua yakuwa ili jambo lao liende kwa mapana ni lazima wao wenyewe waweze kulipa uthamani kwa upana.

Hivyo kwa ukubwa wa Miss Tanzania ilipaswa iwe ni mahala pakutukuza muziki wetu kwa hali ya juu. Na sio nyimbo za Nigeria kutawala kanakwamba ni Miss Nigeria ilihali ni Tanzania.

Jambo hili la kupiga zaidi nyimbo za Nigeria ni jambo lenye fedheha mno lakini sisi hatushangazwi maana  “Kamba hukatika pabovu”.

Basi tuunge kuanzia hapo na tujue kutumia jiwe mosi katika upana wa ndege wawili. Kwa maana nyakati tunasherekea mashindano ya urembo basi pia tupige zaidi nyimbo zetu.

Ila hatuwezi kusahau matumizi ya lugha, hakika fikra kamili huletwa na lugha asili hivyo ni vyema kutukuza Kiswahili na si kingereza. (Fedheha). Yote ya yote tunapongeza upana wa mashindano na wote ambao wameipa hadhi tena Miss Tanzania.

#TuzungumzeMuziki