HAWA WASANII WAMETUACHIA FIKSI MPAKA LEO

Na John Simwanza

Tumesha zoea na imekua ni kawaida kwa msanii kuweka wazi mipango na malego yake ya mbeleni ili mashabiki angalau wapate kujua machache yatakayo jiri kwa msanii wao.

Lakini huwa inakuja kuwa ni tofauti pale tu mashabiki wanapoona muda unazidi kwenda na lolote halionekani na wakati mwingine msanii harudi tena kwenye media kuzungumzia ahadi yake imekwamishwa nanini hii huwa inamtengenezea mazingira magumu sana msanii kwa mashabiki wake nakuonekana kuwa ni mtu wa fiksi.

Wasanii wakubwa hasa ndio wenye haya mambo ya kutangaza vitu vizuri lakini mwisho wa siku wanaacha kile walicho kiweka wazi kwa hadhira na kuibuka na vitu vingine kabisa kutokana na hayo nina haki ya kumuuunga mkono fid q kwa msatari wake usemao “Inaboa sana kuvaa jezi nyingi na wala sikufichi”hata mi siwafichi wasanii inawaboa sana mashabiki mnapokua mnarukia kitu kingine kabla haujamaliza kilichokua kwenye mipango.

Ahadi zipo nyingi sana walizo ahidi wasanii kwa mashabiki wao na mpaka Leo ukiwauliza bdao wanasema kuwa wapo kwenye Mipango ambapo ni tofauti kabisa na muda waliotoa wakati wanapo utambulisha mladi kwa mashabiki wao acha tuziangalie ahadi zilizokua na mtazamo wa mafanikio mbeleni endapo wangezitoa.

AFANDE SELE (MFUNGWA) Ndio mmiliki halali wa taji la mfalme wa Ryhmes mpaka sasa ililofanyika Mara moja tu lililokuwa limeandaliwa na kampuni ya Global publishers.Afande sele anamuda usiopungua miaka miwili kama sio matatu hajasikika hewani na kazi mpya pengine ni labda kutokana na kuwa na mambo ya kuusaka ubunge wa morogoro mjini lakini ni mwaka sasa umepita tangu uchaguzi kupita na hakutangaza kuachana na muziki na Mara ya mwisho alipewa nafasi kubwa namuda wakutosha kuzungumzia muziki na kituo cha East Africa Radio kwenye kipindi cha planet bongo “Heshima ya Bongo flava” Mengi aliyazungumzia lakini kubwa ni kuachia ngoma yake mpya alioipa jina la Mfungwa na alitoa muda kuwa ndani ya wiki mbili ataachia kazi hiyo iliyofanywa na mpishi mashuhuri nchini P funk Majani lakini mpaka Leo hii ngoma haijatoka na pengine angeitoa kazi hiyo huenda ingekua ni miongoni mwa ngoma ambazo zinge ishi miaka mingi kutokana na uandishi wa Afande ambao huwa unamgusa Kila mmoja kwa nafasi yake lakini afande Sele amekuwa kimya sana kulizungumzia hili hiyo niwazi kuwa Mfalme sele ametuachia fiksi mpaka sasa.

JOH MAKINI & NIKKI WA II (BEI YA MKAA ALBAMU) Hawa ninaweza kuwaita ni miongoni mwa wasanii ambao hawatakuja kusahaulika milele na milele katika muziki wetu wa hip hop hapa Tanzania hawajaanza Jana tu kufanya kazi wakiwa pamoja ni wanamuda mrefu tangu Niaje ni vipi, Higher mpaka nje ya Box hizo ni chache tu lakini kazi iliyo wasisimua wafuasi wa wanandugu hawa wa damu nyingine ni bei ya mkaa ilio kuwa stori Kila kona na mashabiki wakataka kujua kipi kitaendelea baada ya bei ya mkaa wawili hai kwa nyakati tofauti walikua wakijibu kuwa huo ni Mradi wao wa kutengeneza Albamu ya pamoja huku wakitoa jina la albamu hiyo itaitwa bei ya Mkaa chakushangaza mpaka muda huu bei ya mkaa haijafanyika na ninaamini kuwa Albamu hii ingetoka nazani ingezidi kuwatengenezea wasifu mzuri sana katika muziki wao bila kujali mauzo yake yangekua vipi.

STEREO (MLADI WA KURUDIA NYIMBO)

B boy stereo kama anavojulikana au Singasinga ni miongoni mwa ma rapa wenye elimu na uwezo mkubwa wa kurap pia anaiwakilisha vyema familia kubwa sana ya Tamaduni muziki inayofanya muziki wa hip hop. Stereo aliibuka na wazo zuri la kuzifufua tena nyimbo zilizowahi kuimbwa na wakongwe mbalimbali hapa nchini na kuzitengene kama Albamu flani ivi ya Old school yenye michano ya kisasa na miongoni mwa kazi alizo kuwa anafikilia kuzirudia ni pamoja na Muda ya joh makini mwamba wa kasikazini na alibainisha wazi kuwa baadhi ya msanii amesha ongea nao na wamempa ruksa akiwemo Ngosha the don ali maarufu Fid q na mpango huo huenda ungekuwa na mafanikio makubwa kwani wakongwe ambao kazi zao zimerudiwa wangeonesha ushirikiano mkubwa sana na kuzisukuma kadri wawezavyo ili kuona imefika mbali na pengine kuvuka mipaka lakini imekua ni kimya mpaka leo na hatujaona wala kumsikia stereo akilizungumzia hilo japo anasikika katika kazi zake zingine na kupelekea mashabiki wake waone amewafanyia fiksi tu.

Nazani ni muda wenu sasa wakua wawazi ili mashabiki wasibaki na maswali mengi ambayo yanaweza yakawa yanajirudia na wafuasi wenu wanawaamini sana na ndio mana mpaka leo wapo na nyinyi hivyo basi msisite kuwapa changamoto zinazofanya wasipate walichokua wanakisubiri kuriko kukaa kimya.