Hatuwezi kuendelea kimuziki kwa kuifitini Tigo Fiesta. (Kweli

Hatuwezi kuendelea kimuziki kwa kuifitini Tigo Fiesta. (Kweli)

Imekuwa ni siku mbaya kwa mtu yoyote mwenye kujua thamani ya jukwaa la Fiesta. Ambapo kwa sasa lina miaka takribani 19 tangu uzao wake.

Na amini twanena yakuwa hakuna msanii yoyote yule wa Bongo Fleva/ Hiphop ambaye hakuwahi kuwa na ndoto ya kufanya Fiesta. (Uhalisi).

Kama yupo na ajitokeze apinge? Nani wakupinga? ilihali ni uhalisi wenye uhalisia ambao tunaujua vyema. (Uhakika)

Na daima tupende kweli jamani, mpaka sasa bado hakuna tamasha lenye ujazo kamili mithili ya Fiesta hii iko wazi. (Ndiyo)

Jukwaa hili limefungua milango kwa wasanii wote shiriki, na linaendelea kufanya hivyo kila

leo. (Kabisa)

Na tunatamani mno matamasha mengine mengi yaje na yawe na ujazo wa Fiesta kwa upana katika ukuzi wa muziki wetu. Maana hata mswahili hunena “Kidole kimoja hakivunji chawa”

Na Whozu, Jay Melody, na wengine wengi kwa hakika wamefunguliwa vyema Dunia ya burudani katika muziki huu kupitia Fiesta. (Vilivyo)

Leo hii katika uwanja wa Learders kungekuwa na vijana wengi katika upya wa ajira ya muziki

kwa maana ya Super Nyota. (Iko hivyo)

Young Killer, Ruby, Nchama, na Edu Boy ni mifano hai na halisi katika Super Nyota tokeo Fiesta. Leo hii uzuio umefanya kukosa kwa watu wengine wa aina hii. (Fedheha)

Lakini upana wa kukosesha mapato katika ngazi ya msanii na wafanyabiashara wengine. Ni chekesho kubwa kuona mdau au msanii akishangilia hili. (Soni)

Na ambao mnasema Fiesta bora ife mnadhani Wasafi Festival na Mziki mnene yatatosha kuchukua wasanii wengine wengi? (Ulizo)

Tujenge ushindani wa maana katika biashara sio fitna zenye fitna kwa kuwa huyu ana nguvu ya ushawishi kwa mwenye mamlaka na huyu hana. (Ujinga)

Tushindane kwa bidhaa sokoni, lakini kama tunaenda kwa upepo huu hakika twanena fedheha ijayo itakuwa kubwa. (Uhalisi)

Na ni vyema watu wajue yakuwa “Sameheo ni lazima, lakini kisasi kindani ya mtu katika haki” (Uhalisia) 

Lakini Clouds wanapaswa kujua yakuwa “Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, hutandika wavu wa kuitega miguu yake” (Tafakari)

Pole zetu ziende kwa Clouds Media Group, tunajua ni watu makini kupita umakini na hii haiwezi kuwavunja moyo katika endelezo la Fiesta 20 hapo 19. (Ujasiri)

Na tunajua mnajua yakuwa “Ukimuona mdudu acheza barabarani na hana mabawa jua shimo lijirani (Ni muda tu)

Mwisho wa siku ni kwamba “Mbio za sakafuni huishia ukingoni”  Mswahili na hekima hunena uhalisia huo. (Ndiyo)

Tafakari…. Hongereni kwa Fiesta ya 2018, mmefanya kwa ukubwa mno. 

#TuzungumzeMuziki