Hatimaye unabii wa Afande Sele juu ya Saida Karoli umetimia.

Hatimaye unabii wa Afande Sele juu ya Saida Karoli umetimia.

“Mimi nilijua Saida Karoli ni mwanamuziki  bora wa kike Afrika, mimi nafahamu sio Tanzania.Saida Karoli yupo juu ya dada yangu Jide, Saida Karoli anajua sijui kuliko Vanessa Mdee anakuwa msanii leo hii.

Unamuacha Saida Karoli unamuamini Vanessa Mdee ambaye anamuiga Beyonce sijui anamuiga Rihanna mimi nasema huu ni upumbavu wa aina yake, kwaiyo leo Vanessa Mdee anakuwa juu kuliko Saida Karoli ni Uchawi”.

Hayo ni maneno ya Mfalme wa Afande Sele ambapo aliyazungumza Tarehe 23/4/2017 nyumbani kwake Mkoani Morogoro pale ambapo Team Tizneez tulifika na kupata fursa ya kuzungumza mengi yahusuyo muziki.

Baada ya kuweka mahojiano haya hoja nyingi zilizuka kutoka kwa mashabiki, wachambuzi wa muziki na wadau mbalimbali wa muziki.

Wapo ambao hawakuficha hisia zao na kuzionyesha hadharani kupinga kauli ya Afande Sele Iliyosema “Mimi nilijua Saida Karoli ni mwanamuziki  bora wa kike Afrika, mimi nafahamu sio Tanzania.Saida Karoli yupo juu ya dada yangu Jide, Saida Karoli anajua sijui kuliko Vanessa Mdee anakuwa msanii leo hii.

Wengine walifika mbali na hoja ya kusema Afande Sele anachuki tena avuliwe ufalme wake.

Jambo hili sisi kama Team Tizneez lilitushangaza mno, kwa maana ni Tanzania pekee msanii akisema jambo Fulani kuhusu msanii mwingine huonekana anachuki, inaonyesha ni jinsi gani wengi hawajui maana ya neno mtazamo. (Maoni)

Miongoni mwa wale waliopinga kauli ya Afande Sele hawakuwa na hoja madhubuti za kuikosoa kauli hiyo bali walishinikizwa na mihemko na mahaba yao binasfsi kwa wasanii walioguswa na kauli ya Afande Sele.

Ingawa ukimsikiliza kwa makini Afande Sele alitete hoja yake ya ubora wa Saida Karoli.

Hivi karibuni umeibuka wimbo mpya wimbo unaozungumza ubora wa Saida Karoli, wimbo ambao awali Afande Sele aligusia kibwagizo tu ikawa shida na gumzo.

Wahenga wanasema atakayemlipa mpiga zumari ndiye atakayechagua wimbo. Safari hii Clouds Media Group wamemchagua Saida Karoli.

Mbiu zinasikika kila kona kuidhihilishia hadhira juu ya ubora, uwezo,ukongwe na mchango wa Saida Karoli katika Sanaa yetu.

Bado tunaishi juu ya maneno ya Afande Sele na kama angerudia Mtazamo hakika kungekuwa na mistari kuhusu Saida Karoli.

Zidume fikra sahihi za Mfalme Afande Sele.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa