Hata saa mbovu wakati fulani husema ukweli (SINGELI) Sehemu ya II

Soma sehemu kwanza hapa chini..

http://tizneez.com/makala/hata-saa-mbovu-wakati-fulani-husema-ukweli-singeli-sehemu-ya-i/

Sehemu ya pili endelea hapa chini..

Hata saa mbovu wakati fulani husema ukweli (SINGELI) Sehemu ya II

Singeli ni mfano ulio bora wa saa mbovu ambayo katika wakati huu imeweza kusema ukweli.

Yanini tufichane ukweli ilihali ‘ukweli utatuweka huru’ Hoja za aina Fulani ya muziki sio biashara zimekuwa zikichukua nafasi kila leo, ila katika ukweli si kweli maana hakuna muziki usiokuwa biashara.

Isipokuwa ni Tanzania  pekee biashara ya muziki anapanga mtu mmoja tena kwa mapenzi yake, amini usiamini ni wazi mashabiki wengi wanapangiwa cha kusikiliza bila wao kujua kama wanapangiwa. Huku wenye kupanga kujisifu katika vijiwe vingi vya muziki “Tukiaza watafuata/watasikiliza’

Singeli ni muziki ambao umeibuka miaka miwili kama sio mitatu nyuma na umeweza kuchukua nafasi kubwa katika matumbuizo mengi hata katika mitaa iliyomingi. Ila muziki wa kizazi kipya upande wa hiphop ni muziki ulionza miaka Zaidi ya 25 nyuma. Na hata uzao wa Bongo fleva ni uzao halali wa muziki wa hiphop.

Lakini uongo mtamu wenye kuaminika na wengi sasa yakuwa hiphop haiuzi umeweza kuchukua nafasi njema katika vyombo vya habari vingi tu.

Lakini katika ile kweli hata ambao wanasema hiphop haiuzi hatujui kipi ni kipimo chao cha kuwa hiphop sio biashara. Katika ile kweli dunia yote hakuna muziki usiokuwa biashara, bali biashara yoyote inahitaji matangazo makubwa ili iweze kuonekana vyema.

Sasa leo kama hiphop itapewa nafasi ipewayo singeli ni wazi itakuwa bishara kubwa mno katika nchi hii.

Licha ya maneno na kukosa nafasi kubwa ila bado nguvu ya hiphop inaendelea kuonanekana katika majukwaa mengi hapa nchini.

Itaendeleaaa

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa