Hata saa mbovu wakati fulani husema ukweli (SINGELI) Sehemu ya I

Man Fongo Ft Sholo Mwamba - Namsaka Panya  Mp3 Music Download [New Song]

Hata saa mbovu wakati fulani husema ukweli (SINGELI) Sehemu ya I

Ni nani muongo wa moja kwa moja katika maisha yote? Ni uwazi kuna wakati ukweli utaonekana bila kificho mbele ya maisha yetu. Lakini jamii inapaswa ifahamu kuwa ‘’jambo baya halikosi walau chembe ya faida’’.

Ujinga hauonekani kwa macho, ila mara pale mjinga anapofungua kinywa chake na kusema ujinga wake. Na wenye utashi kujua kuwa huu ni ujinga baada ya kupima maneno yake, ndipo tunapojua kwa kina kuwa huu ni ujinga. Ni mara chache mno ujinga kudhihirika kwa vitendo.

Cha ajabu katika nyakati hizi wajinga wachache wameweza kuwateka wale ambao tulikuwa tukiwaamini kila leo juu ya werevu wao. Lakini kila sekunde,dakika, saa, hata siku ujinga umeendelea kuwatawala hata sijui wamenunuliwa kwa bei gani ili tu kwenda sawa kasi ya ujinga.

Ujinga wa kuwaaminisha wasanii wa hiphop wabadilke ndio wapate pesa umeendeleaa kukua kila leo.Ila siku zote kukata tama na kutokuwa na misimamo ni sifa kubwa ya wajinga. Je hao walioamua kubadilika kweli wamepata hizo pesa?

Singeli ni mfano uliobora wa saa mbovu ambayo katika wakati huu imeweza kusema ukweli.

Yanini tufichane ukweli ilihali ‘ukweli utatuweka huru’ . …..

Itaendeleaaa

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa