Harmonize hafai na hana sifa kuwa jaji kwenye kutafuta watangazaji.

Harmonize hafai na hana sifa kuwa jaji kwenye kutafuta watangazaji.

Yanini tufichane ukweli ndugu zetu? Ni vyema tuambiane ukweli maana licha ya kuwa huru lakini kweli itafanya watu wajitambue.

Tumeona namna ya ufunguliwaji wa vituo vya habari vya msanii Diamond Platnumz na hamasa imekuwa kubwa kwa vijana wengi kuona ni jambo jema na zuri.

Na moja ya vitu ambavyo tumevipenda kutoka nyumba ya Wasafi ni kuingia mtaani kutafuta watangazaji ambao wanatazama vipaji Zaidi na si vyeti lakini kutafuta wapya na sio ambao huwasikia kila leo.

Na amini jambo hili ni zuri kwa maana akitengeneza vijana wake kutakuwa na watangazaji wenye uchungu juu yake Wasafi Radio na Runinga.

Lakini katika makosa afanyayo yeye na uongozi wake ni kumueweka Harmonize jaji kwa upande wa kuchagua watangazaji leo Visiwani Zanzibar.

Harmonize ni msanii ambaye hata matamshi ya silabi kwenye kinywa chake hayakai sawa, lakini hata uandishi wake wa kwenye mitandao ya kijamii hauko sawa je!mtu huyu anawezaje kuwa jaji wa kujaji kwenye upande wa watangazaji?

Mtu ambaye hajui tofauti ya R na L au N na M anawezaje kuwa jaji? Ni wazi yapasa Wasafi wajitafakari katika muendelezo wa mchakato huu.

Kuna watu wengi wengi mno wa kuwatumia katika mchakato huu ambao wako sawa na ubora katika uwanja huu wa utangazaji.

Mtu kama Taji Liundi, Fredrick Bundala, Ezden the Rocker, Carol Ndos, Daniel Kidjo,Salama Jabir, John Dilinga, Dee 7  na wengine wengi ni wazi wangepata watu bora Zaidi katika mchakato huu.

Ni wazi hata Diamond Platnumz hafai kuwa jaji katika mchakato huu maana uwepo wake utafanya wengi kuto kuwa huru katika maamuzi yake lakini pia hawezi kujua undani wa mtu mwenye kutangaza.

Ni vyema wangechukua watu wenye taaluma hiyo au wenye uzoefu wa kujua undani wa uzao wa utangazaji.

Semi ya mswahili hunena “Ukijua upande huu upande huu huujui” na wakati huo “Hasara humfika mwenye mabezo”

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa