“Hamorapa mfano wa kichwa cha kuku kisichostahimili kilemba”

“Hamorapa mfano wa kichwa cha kuku kisichostahimili kilemba”

“Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe” Msemo huu unaenda sawa na kasi ya mwenendo wetu sisi kama Tizneez. Maana katika uhalisia sisi sio watu wa kuweka vitu vya kipuuzi bali kukemea bila kujali nani ni nani.

Na haitumizi mikono yetu kama wengi wafikiriavyo ila kusimamia ukweli inatupa nguvu kwa maana ya kupata uhuru kwenye kuhubiri kweli yenye kweli.

Jambo hili limetujengea utofauti mkubwa baina yetu na blog nyingine. Na wala haitupi chukizo bali kusimama katika kile ambacho tunaamini kina maana leo na kesho.

Wakati wengine wakiamini kiki na udaku ndiyo kitu pendwa kwa mashabiki wengi sisi imekuwa ni tofauti kabisa kwa maana ndiyo kwanza tumeanzisha kampeni ya #ZimaKikiWashaMuziki.

Lakini hoja ya kiki na udaku usio na maana imeendelea kukua kwa maana hata wale wachambuzi wengi na watangazaji wengi wamekuwa wakiipa nguvu njema tendo la kiki na udaku wake.

Ni wazi kiki inarudisha nyuma muziki hili halina kificho, lakini kiki hupita kiwepesi kama usiku wenye raha.

Mfano tosha wa kuisha kirahisi na kupita kiwepesi ni Harmorapa. Ambaye kiki zilimtoa vyema lakini katika uhalisia si msanii ambaye alipaswa kupata muda wa hewani kama ule ambao alipata, ila tupo kwenye mfumo wa watu ambao wanaamini kwenye kiki Zaidi. Ila Harmorapa hakuna uwezo wa kisanii ambao aliweza kuonyesha mara alipopata nafasi kwenye uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Hakika daima “kichwa cha kuku hakistahimili kilemba” hivyo haishangazi hata kidogo kupita alivyopita maana ni wazi umeona wapi kuku amevaa kilemba?

Njia pekee ya kumrudisha kwenye midomo ya watu sio kiki tena bali kazi yenye uwezo wa kwenda kasi na muziki wa sasa.

Maana katika ule upana ni wazi mazoea ya kiki juu yake yameshatawala kwa maana hakuna kiki ambayo itawafanya watu wazungumzie kama awali.

Tusiache kusema ile kweli yenye ambayo itasaidia kukuza na kueneza vyema muziki wetu kila iitwapo leo. Kwa maana “Asali na shurubati haina ladha moja”

#ZimaKikiWashaMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa