Hakuna sifu itakayoweza kuwa zaidi juu ya Joh Makin. (Uhalisia)

Hakuna sifu itakayoweza kuwa zaidi juu ya Joh Makin. (Uhalisia)

Ukirejea katika usikivu wa wimbo wake wa ‘Zamu Yangu’ ambao sasa una miaka takribani 10 na zaidi ni wazi huwezi kupata neno kuu la kusifu katika uwezo wake. (Mwamba)

Joh ananena katika wimbo huu wa ‘Zamu Yangu’ yakuwa ” Hata dhahabu haifikii thamani ya kipaji changu”. Lakini pia “Makini daima kinachonibeba ni rhymes zilizo kali, Jicho langu la tatu linaona mbali” (Zamu Yangu)

Kwa hakika ni uhalisia wenye ukuu, kwa maana ujazo wa mitambao na uandishi ni katika upana mkubwa. (Ujuzi)

Tangu ‘Hao’ mpaka ‘Mchele’ ya  sasa akiwa na Lunya inaonyesha kwa ukubwa wa thamani ya kipawa chake. (Hakika)

Ni wazi Joh hajawahi kuchosha tangia tangu na tangu katika usikivu, na hii ni uwezo wa kubadilika vyema katika wimbo. (Naam)

Na mabadiliko ya kisanaa ni ugonjwa usiotibika kwa wasanii wengi wa hiphop. Ilihali Joh ni mwenye ubadiliko katika tosha ya ujazo mkuu. (Ujuzi)

Mchele ni uhalisia katika badiliko kamili, usikivu ni wenye burudisho kuu katika nyakati zote kwa maana ya asubuhi, mchana, alasiri, jioni kadhalika usiku. (Hakika)

Na wimbo wowote wenye kuweza kusikilizwa katika nyakati zote ni wenye thamani zaidi. Joh amekuwa ni mwenye nyimbo nyingi katika usikivu wa nyakati zote. (Uimara)

Ni wazi hatuna sifu ambayo tutaeleza na ikatosha kwa Joh Makin, isipokuwa kushukuru kuwa nae katika muziki huu. (Shukurani)

Na tunasifu kwa uwazi katika kusema haya kwa maana “Inapaswa usifu moyoni mpaka machoni” (Daima)

Joh anabaki kuwa msanii bora wa HipHop mwenye uwezo kamili na asiye na robo ya hovyo bali sanaa yake kwa upana kamili. (Pongezi)

Na ambao wanaona Joh hashiriki katika mijadara mingi ya HipHop na maugomvi mengi warejee usikivu wa Wimbo wa ‘Mfalme’ majibu yote yapo hapo/kule. (Hakika)

Yote ya yote tuendelee kufurahia juu ya ‘Mchele’ maana hakuna nyingine katika usikivu imara sasa. Na “Ngurumo ya mitambo katika wimbo huu wa ‘Mchele’ ni mithili ya Simba Dume lenye manyoya mengi shingoni” (Naam)

#MuzikiNiSisi